Mkuu wa Shirikisho la Shuti atangaza kupokea Misri kwa kombe la dunia kwa Kibweta cha risasi
- 2020-09-05 10:29:28
Jenerali Hazem Hosny Mkuu wa mashirikisho mawili ya shuti ya Kimisri na Kiafrika , alitangaza kukubali kwa shirikisho la kimataifa la shuti kwa kupokea ubingwa wa kombe la dunia la shuti kwenye sahani ( Kibweta cha risasi ) kuelekea Misri ili kufanyika kwenye ardhi ya mafarao mnamo Februari 26 hadi Machi 8,2021 , kwa ushiriki wa idadi kubwa ya wapiga shuti duniani kote .
Hosny akiashiria kuwa Misri itapokea pia ubingwa wa dunia wa shuti kwa vijana na wasichana kwa bastola na bunduki , utakaofanyika mwaka wa 2023 katika moja muhimu zaidi ya shughuli za mchezo.
Akasema : " nashukuru wizara ya vijana na michezo na kamati ya olimpiki ya kimisri kwa ufadhili unaolisaidia shirikisho la shuti kufanikisha mashindano hayo "
Akaelezea kuwa shirikisho liko tayari kwa sura kubwa kupokea ubingwa huo, akisisitiza kuwa Misri ilikuwa inakaribisha mashindano makubwa kwa kiwango cha kiarabu , kibara na kimataifa mnamo miaka iliyopita, tuna uzoefu na uwezo, jambo linalotusaidia kuwa na sura bora zaidi .
Mkuu huyo alisisitiza kuwa kupokea mashindano makubwa,ni jambo lenye matokeo kwenye kiwango cha kimataifa , na tena linakuza utalii nchini Misri kwa sura kubwa , pamoja na matokeo ya kiufundi yatakayokuja kwa wachezaji wamisri kupitia kutoa fursa za kukabiliana na wapiga shuti bora zaidi duniani , na kuongeza uzoefu wao .
Comments