Misri yapeleka ujumbe mkubwa zaidi wa Amani ulimwenguni

Waogeleaji 550 huwakilisha alama ya Amani ya ulimwengu kwenye maji ya Mfereji wa Suez.

Katika mfumo wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Amani ya Kimataifa mnamo Septemba 21 ya kila mwaka, ili kuimarisha maadili ya amani kati ya watu na mataifa yote, na kuizingatia siku hiyo kama siku ya kukataliwa kwa vurugu na kusitisha mapigano, Misri inapeleka ujumbe mkubwa zaidi wa Amani ulimwenguni chini ya usimamizi wa Wizara ya Vijana na Michezo na Shirikisho la Kuogelea na ukoaji  la Misri na Mamlaka ya Mfereji wa Suez, ambapo waogeleaji wa Misri 550 huwakilisha alama ya Amani duniani kwenye maji ya Mfereji wa Suez, wakisisitiza kuwa utamaduni wa amani ni utamaduni wa mazungumzo na ulinzi kwa watu na maendeleo yao, na hakuna njia ya kufanikisha maendeleo endelevu bila Amani.


Mwaka huu wa 2020 ni wazi kwa hakika inayosema kuwa sisi sio maadui wenyewe kwa wenyewe.Lakini, adui wetu wa pamoja ni virusi visivyoacha kutisha afya yetu, usalama na maisha yetu bila kuchoka, wakati ambapo Janga la Corona "Covid 19" limeiweka dunia yetu katika hali ya fujo, na limetukumbusha kuwa linalofanyika katika mahali pamoja Duniani linaweza kuathiri watu wote mahali popote.


Kupitia hafla hii, Misri inatoa wito kwa mataifa na watu wote kujitolea kukomesha mapigano, na Misri itatuma ujumbe huo ulimwenguni kwa kuanzisha changamoto mpya  inayozidisha na kuimarisha dhana ya siku hii kwa kueneza utamaduni wa huruma, rahma na matumaini mbele ya janga hilo, ambayo ni utekelezaji wa ishara kubwa zaidi ya amani  kwenye Maji ya Mfereji wa Suez mjini Ismailia.



Waogeleaji 550 wa Misri wanashiriki katika changamoto hii chini ya uongozi wa bingwa wa kimataifa Nahodha Walaa Hafez na mbele ya timu ya usuluhishi ya kimataifa kutoka kwa shirika la Guinness World Record, litakalofanyika mnamo 9/21/2020 (Siku ya Amani duniani).


Imeamuliwa kuwa maelezo yote yatatangazwa katika mkutano wa waandishi wa habari mbele ya vyombo vyote vya habari vya ndani na vya kimataifa.


Ikumbukwe kuwa tukio hilo linakusudia kufikia rekodi mpya ya ulimwengu kuvunja rekodi ya ulimwengu inayohakikishwa na waogeleaji 460.


Comments