Ahmed Al-Ahmar : Lengo la Misri ni kuwafurahisha mashabiki katika kombe la dunia la mpira wa mikono

Ahmed Al-Ahmar, nyota wa kilabu cha Zamalek na timu ya kitaifa ya Kimisri ya mpira wa mikono, alisisitiza kuwa lengo la nchi yake katika Mashindano ya Dunia ni kuwafurahisha Wamisri katika mashindano yatakayofanyika nchini Misri mnamo kipindi cha tarehe 13 hadi 31, Januari ijayo.


Nimefurahishwa na mazingira na kukutana na nyota wengi wa mchezo huo, na ninaamini kwamba timu ya kitaifa itafanya bidii ili kuwafurahisha mashabiki," Al-Ahmar alisema katika taarifa pembezoni mwa sherehe ya kura ya michuano.


Nyota huyo wa timu ya kitaifa ameongeza: "Hatufikiri juu ya kundi ambalo tutaingia, kwa sababu tunatarajia mechi ngumu, na lengo letu ni kufikia utendaji na matokeo yanayofaa mpira wa mikono wa Misri."


Al-Ahmar alishiriki kwenye kura ya Kombe la Dunia Jumamosi, huko eneo la Piramidi, pamoja na Abdul Rahman Homyd,  aliyeshinda lakabu ya  golikipa bora zaidi katika Mashindano ya Dunia ya Vijana huko Macedonia, pamoja na Hassan Kaddah, aliyekuwa mfungaji bora katika mashindano ya ulimwengu.


Misri itakaribisha michuano ya kombe la dunia la mpira wa mikono katika toleo lake la 27 mnamo kipindi cha tarehe kutoka 13 hadi 31 Januari 2021, kwa ushiriki wa nchi 32 kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo.

Comments