Ujumbe wa Shirikisho la kimataifa na Sport five zatembelea kumbi za kombe la dunia la mpira wa mikono, Misri 2021

  Ujumbe wa Shirikisho la mpira wa mikono la kimataifa na mdhamini wake, Sport Five, zilitembelea kumbi za toleo la 27 la mashindano ya mpira wa mikono ya dunia kwa wanaume, Misri 2021.


 Ujumbe huo ulianza ziara zake kwa ukumbi wa  6 Oktoba, na utaendelea kutembelea kumbi zilizobaki wakati wa siku zijazo ili kuhakikisha kuwa kumbi hizo ziko tayari kabisa kwa ajili ya  uandaaji wa tukio hilo la kimataifa.


Na hapo awali, Hussein Labib, mkurugenzi wa mashindano ,kwa tovuti rasmi ya Misri 2021, alisema kuwa " Oktoba 31 ni tarehe ya utayari wa kumbi zote nne kwa ajili ya kuandaa mechi, na uratibu kati ya kamati zote utafanywa kwa ajili ya mashindano yanafanyika kikamilifu".


 Pia, Waziri wa vijana na michezo Dokta.Ashraf Sobhy alisema kuwa utayari wa kisasa wa kumbi hizo ulifikia 88%, mwanzoni mwa mwezi huu.


Na jumamosi, Kura ya mashindano ilifanyika katika mazingira ya ajabu huko eneo la Piramidi za Giza.


 Na mashindano hayo yatafanyika kuanzia tarehe  13 Januari ijayo hadi 31 kwenye kumbi nne, nazo ni uwanja wa Kairo, 6 Oktoba, mji mkuu wa kiutawala na Borg Al Arab.



Comments