Kocha wa timu ya taifa ya Uswidi: kuchagua Misri kunatuhimiza, na ninadhani kuwa sisi ni bora zaidi katika kikundi chetu
- 2020-09-13 15:36:06
Kocha wa timu ya taifa yaUswidi “Glenn Solberg ” anaona kuwa timu yake lazima kuwa timu bora zaidi katika kikundi chake katika toleo la 27 kutoka mashindano ya dunia ya mpira wa mikono ya wanaume- Misri 2021.
Timu ya taifa ya Uswidi iliyoshinda mashindano kwa mara nne kabla ya hivyo iliwekwa katika kikundi cha saba, pamoja na timu ya Misri –mwenyeji -, timu ya Ucheki, na timu ya kuiwakilisha Marekani kusini -itakayochukuiwa baadaye.
Mswidi Solberg amesema: “kukabili timu ya Misri nchini Misri ni jambo gumu, lakini kuchahuliwa kwao kwa kucheza dhidi yetu ni jambo linalotuhimiza”.
Akaongeza: “jambo linategemea kwenye msimamo wa kuhudhuria kwa watazamaji. Kucheza katika ukumbi unaojaa na watazamaji mjini Kairo bila shaka litakuwa jaribio zuri sana”.
Akakamilisha: “pia, timu ya Ucheki ina wachezaji wanaovutia, na imepata kiwango cha sita katika mashindano ya mataifa ya Ulaya, mwaka 2018”.
Akasisitiza: “kila kikundi kina timu mbili au tatu nzuri sana, lakini ninadhani kuwa timu yetu lazima kuwa bora kuliko zote”.
Ama Mkuu wa timu “Jim Gotfreidson” amesema: “ninapenda kucheza mashindano ya kikundi, na ninataka kuiwakilisha Uswidi nchini Misri”.
Akakamilisha: “kucheza dhidi ya Misri kwenye ardhi yake na jaribio zuri sana, na ninadhani kuwa fainali ya kikundi itakuwa baina yetu na timu ya Misri”.
Akahitimisha: “pia, tuna heshima kubwa kwa timu ya Ucheki”.
Comments