"Infantino" na Ghada Wali wasaini mkataba wa makubaliano ya kumaliza ufisadi na uhalifu katika michezo

Giani Infintino Mwenyekiti wa Shirikisho la kimtaifa la Soka (FIFA) alisaini mktaba wa mkabiliano pamoja na Ghada Wali, Mkurugenzi mtendaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa kupigana na uhalifu na Madawa ya kulevya , ili kutumia michezo kupambana na Uhalifu. 


Akaunti rasmi ya FIFA kwenye Twitter ilichapisha picha ya Infantino na Ghada wali na iliandika "Rais wa FIFA  na Mkurugenzi  mtendaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na Madawa ya Kulevya na uhalifu Ghada Wali huko Vienna, walisaini mkataba wa mkubaliano ili kumaliza ufisadi na uhalifu katika michezo ,  Ushirikiano wa pamoja unashughulika kutumia mpira wa miguu kama njia ya kukuza uwezo wa vijana kukabiliana na uhalifu na utumiaji wa Madawa ya kulevya na kuwafundisha ujuzi wa maisha"


Wali alifanya kazi kama Waziri wa Mshikamano wa kijamii huko Misri na alikuwa msimamizi wa kampeni ya "Wewe ni mwenye Nguvu zaidi kuliko Madawa ya Kulevya" ambayo bingwa wake  alikuwa bingwa wa kimataifa wa kimisri Mohamed Salah , mchezaji wa Liverpool ili kupigana na Madawa ya Kulevya.

Comments