Waziri wa michezo atangaza maelezo ya alama kubwa zaidi ya Amani kwenye maji kwa kushiriki na waogeleaji 500

Waziri wa michezo: sherehe ni ujumbe wa Amani kutoka nchi ya Misri kwa watu wa Dunia wanaopenda Amani.


Waziri wa michezo: watu 200 wenye ulemavu  watashiriki katika sherehe. 


 Adhuhuri ya jumatano, katika mkutano wa waandishi wa habari kwenye makao makuu ya wyizara ya vijana na michezo Dokta Ashraf Sobhy –Waziri wa vijana na michezo- aliyatangaza maelezo ya sherehe ya kimichezo kwa kufanya alama kubwa zaidi ya Amani kwenye maji, pamoja na kuhudhuria kwa Sameh Al Shazli , Mkuu wa Shirikisho la kimisri kwa kupiga mbizi na kuokoa wa kimisri-, na Nahodha Walaa Hafidh –Mwongozo wa mamlaka ya mfereji wa Suez.


Sherehe ya kimisri itafanywa pamoja na sherehe za mataifa za siku ya Amani ya kimataifa, na inayokuwa mnamo siku 21, Septemba kila mwaka. Inajumuisha kurekodi alama kubwa zaidi ya Amani kwenye maji, na kusajili waogeleaji 500 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni katika Elezo la Guinness la rekodi, ili kuvunja rekodi ya kituruki iliyosajiliwa kwa waogeleaji 460. Sherehe itaandaliwa kwenye maji ya ziwa  la Mamba  mkoani Ismailia.


Dokta Ashraf Sobhy –Waziri wa vijana na michezo- alisisitiza kuwa sherehe ni kama ujumbe wa Amani, upendo, fahari kwa ulimwengu, na mwaliko kwa ulimwengu ambao msingi wake mkuu ni Utulivu na Amani, akiashiria kuwa ni msingi muhimu unaounda watu na mataifa.


Waziri huyo aliongeza kuwa sherehe ni ujumbe wa Amani kutoka nchi  ya Misri, ambao Misri inauita kwa mataifa wa ulimwengu katika kila sherehe chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El Sisi –Rais wa Jamhuri- kwa Uvumilivu, kuunga mkono Amani, kupambana na itikadi kali na ugaidi unaosababisha madhara na uharibifu kwa ulimwengu, akiashiria kuwa Misri itakuwa kuungana na ustaarabu na Mtengenezaji wa Amani.


Akisisitiza kuwa Wizara inafanya kazi chini ya maagizo ya uongozi wa kisiasa kwa kuungana na mipango yote ya vijana katika sehemu zote za vijana, michezo, kijamii, na kimaendeleo kwa jumla.


Kwa upande wa Sameh Al Shazli, amesema kuwa tukio ni ujumbe kwa ulimwengu unaosisitiza kuwa Misri ni nchi ya Amani na Usalama.


Nahodha Walaa Hafidh alielekea shukuru na heshima kwa Waziri wa vijana na michezo kuhusu kuunga mkono tukio, akisisitiza kuunga kwa  Misri kwa kila kinachohusu kueneza Utamaduni wa Amani na Utulivu.


Matukio ya sherehe yataendelea mnamo kipindi kutoka Oktoba Mosi hadi Oktoba 6, wakati ule ule wa sherehe za ushindi mtukufu wa Oktoba, ambapo Mji wa Sharm El Shiekh unashuhudia matukio kadhaa, muhimu zaidi ni muda ndefu zaidi ya kubakia chini ya maji ya wanaume kwa masaa 150 kwa kuvunja rekodi ya kiuturuki iliyosajiliwa kwa masaa 142, dakika 42, na sekondi 42, na muda ndefu zaidi ya kubakia chini ya maji ya wanawake kwa masaa 55 kwa kuvunja rekodi ya kimarekani kwa masaa 51, dakika 25. Kama, matukio yanajumuisha mfulizo mrefu zaidi wa binadamu kwa idadi wazamaji 700 kwa kuvunja rekodi ya kiindonesia iliyosajiliwa kwa idadi wazamaji 538.


Waziri huyo alitangaza kuwa vijana 200 wenye ulemavu watazoezewa  ili kushiriki katika matukio yatakayoandaliwa, pamoja na kuchukua hatua zote za Usalama na Ulinzi. Pamja na hatua za tahadhari zilizokubaliwa na Wizara ya Afya ya kimisri kwa kuhifadhi Afya na Usalama za washiriki.

Comments