Mfalme wa Misri katika ulimwengu wa soka

 Mohamed Salah anayejulikana kwa jina la moo Salah . Amezaliwa tarehe 15 mwezi wa 6 mwaka wa 1992 huku Basyon kijiji kimoja kilichopo kilomita 130 kaskazini mwa mji mkuu wa Misri, kairo .Salah alilazimika kupitia tatizo la kusafiri kwa saa 9 kila siku mara nyingine akilazimika kutumia mabasi 10 ili kufikia kituo cha mazoezi mjini Kairo .Amekua katika hali mbaya ya kifedha.Hali hiyo imemlazimika kuyaacha matakwa yake ya kielimu katika kitivo chake lakini hakukata tamaa na amefuala kuhakikisha mafanikio yanayosikika ulmwenguni kote .

Alifungua ukurasa wake katika ulimwengu wa soka katika kilabu Al-Mokawloon baadaye alijiunga kilabu cha Basel inayoshiriki katika ligi ya Switzerland.Basel imemtoa Salah nafasi ya kucheza mpira wa miguu kwa mara ya kwanza barani Ulaya.Baadaye alijiunga vilabu kadhaa kama Chelsea, Fiorentina,Roma na mwishoni Liverpool.

Mwanzo wa mchezaji nyota

Huku wachezaji wakisherehekea kwa fujo baada ya 4:0 dhidi ya Enppi , kocha Said Al Shesheni aliangalia upande mmoja na kugundua kwamba mchezaji mmoja wa timu ya Al-Mokawloon wa timu ya wachezaji wasiozidi umri wa mwaka 16 . Salah alikuwa akibubujikwa na machozi kwamba jina lake halikuwa katika oradha ya wafungaji mbao. Salah alifaulu kuonyesha umahiri wake na kwa sababu hii kocha wake Al Sheheni alimpelekea safu ya mbele na alicheza na timu ya kwanza mwaka 2010.Mechi yake ya kwanza katika ligi kuu ya Misri ilikuwa dhidi ya Al-Mansura.Msimu uliofuata Mohamed Salah alikuwa mchezaji muhimu katika timu ya kwanza.Jambo hili liliyavutia macho ya wafuatiliaji ,wahakiki na wagunduzi wa talenti wa vilabu vingine.Na kwa hiyo kilabu El-Zamalk alijaribu kumsajili lakini El-Zamalk ilikataa kwa sababu ya alikuwa ghali sana kulingana na umri wake.

Mwaka 2012 alijiunga kilabu Basel na hiyo ilikuwa mstari wa kwanza katika ukurasa wake katika ulimwengu wa soka barani Ulaya . Salah alitumia misimu miwili yenye mafanikio na timu ya Basel . Katika msimu wake wa kwanza alifika nusu fainali ya ligi ya Ulaya lakini timu yake ilishindwa kufikia mechi ya fainali. Licha ya hivyo Salah alionyesha umahiri wake katika mchuano huo akifunga mabao mawili dhidi ya timu za ligi kuu ya Uingereza: Chelsea na Tottenham.Salah alifaulu na timu yake kufuzu ligi ya Switzerland lakini timu hiyo ilishindwa katika mashindano ya kombe katika mechi ya fainal.Msimu uliofuata Basel ilishiriki katika kombe la vilabu bingwa Ulaya na kama kawaida Salah alifunga bao dhidi ya Chelsea . Licha ya hivyo timu yake ilishindwa kupata taji lolote msimu huo na hiyo ndio sababu inayomfanya Salah kufikiri kujiunga vilabu vingine na hasa Chelsea na Liverpool

Mwishoni aliamua kuijunga Chelsea msimu wa 2013/2014 .Muda aliyetumia huku Chelsea ilikuwa ngumu kwa sababu ya timu yake ilikuwa inajumuisha wachezaji wa kiwangu cha juu kama Hazard na Willian N.K .Kuingia katika mpango wa kocha JM lilikuwa jambo gumu. Mechi yake ya kwanza na Chelsea ilikuwa dhidi ya Newcastle. Lakini alifunga bao lake la kwanza na Chelsea katika London derby  dhidi ya Arsenal .Msimu huo hakukidhi matakwa ya Salah na Wafuasi wake . Katika mechi  11 alizochezea Chelsea alifunga mabao wawili

Msimu wa pili na Chelsea , hali ya Salah ilikuwa mbaya zaidi.Katika mechi 8 alizochezea alishindwa kufunga mabao.Na kwa sababu hiyo alipelekwa kwa mkopo kwa Fiorentina nchini Italia . katika  muda wa miezi sita Salah alishiriki katika mechi 26 alifunga mabao 9 na alifaulu kuonyesha umahiri wake ingawa ugumu wa calcio

Salah alifufua matakwa yake kabla ya kusainiwa na Roma fc nchi Italia katika msimu wa 2015/2016 .Huko Roma Salah alipata ujuzi na alikuwa mshambuliaji hodari mno. Alikuwa uti wa mgongo wa mpango wa kocha wake Spallitti na katika misimu miwili na Roma fc , Salah alishiriki mechi 83 alizochezea Roma katika mashindano yote akifunga mabao 33 .Msimu wa 2016/2017  Salah alichuguliwa kuwa mchezaji bora wa ya Roma Katika ligi kuu.

Mwaka 2017 Liverpool ilimsajili Salah kwa kitita cha $ 55.7 m .Salah mara hii alifaulu kuonyesha umahiri wake nchini Uingereza . katika mechi 48 alizochezea Liverpool katika mashindano yote raia huyo wa Misri alifunga mabao 43 na kusaidia pasi za baoa 15 .Na pia aliisaidia Liverpool kufika fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu 2007 . Ama msimu huu anaongoza oradha ya wafungaji mabao .

Kwa upande wa timu ya taifa ya Misri Salah alichezea safu zote . Alishiriki katika mashindano mengi na timu ya taifa ya Misri kama kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi , Afcon mwaka 2017 nchini Gabon lakini timu yake ya taifa ilishindwa kufuzu taji baada ya kupigwa 2:1 na Kameruni katika mechi ya fainali na alishiriki katika michezo ya Olimpiki mwaka 2012 nchini Uingereza .

Mambo ya kheri

Salah amelipia ujenzi wa shule na hospitali na kuweka jina lake katika mashirika ya hisani ikiwemo kuchangisha $280.000 kwa hazina ya serikali inayolenga kuimarisha kiuchumi familia za wamisri masikini

Ameshiriki katika kampeni za kuwafahamisha vijana madhara ya madawa ya kulevya .

Mafanikio ya mfalme wa Misri :

Taji la mfungaji bora katika ligi kuu ya Uingereza kwa msimu wa 2017/2018.

Tuzo ya mchezaji bora wa mwaka Afrika 2017 na 2018.

Tuzo ya BBC kwa mwanakandanda bora wa Africa miaka 2017 na 2018.

Mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu wa 2017/2018.

Alikuwa miongoni mwa kikosi bora cha Afcon mwaka 2017.

Comments