Waziri wa vijana,awaheshimu washindi wa kombe la dunia katika mashindano ya vitendo vya wanafunzi kwa kuhudumia jamii
- 2020-09-21 10:34:58
Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo ameiheshimu timu ya wanafunzi wa Al-Azhar waliofuzu kombe la dunia katika mashindano ya harakati ya wanafunzi kwa kuhudumia jamii na Ujasiriamali 2020 kwa timu ya Inakits Misri,matokeo hili yamekuja baada ya kushinda timu 32 zilizoshiriki katika mashindano na zinazowakilisha vyuo vikuu kadhaa ulimwenguni kama Canada,Marekani,Ujerumani,India,China,Korea na Brazilia.
Mradi wa wanafunzi wa Al_Azhar ni kushika faida kutoka takataka hazina faida kama ganda ya uduvi na kuigeuka kwa kitu muhimu: ladha ya uduvi ya kiasili na wanaofanya kazi hii ni wanawake wanaokaa vijijini karibu na kisiwa cha Karun, pamoja na kutengeneza mbolea wa kilimo kutoka gamba ya uduvi inayohusiana na kurutubisha ardhi mara tena.
Na waziri akisifu uchangamfu wake kwa wanafunzi wa Al-Azhar kwa sababu ya ustadi wao wa kielimu, na vilevile wameweza kuhudumia jamii kwa kuweka masuluhisho mapya yanayokuza kufaidikia vitu kwa njia za kielimu,na ufanisi wao katika shindano la kimataifa kwa vitendo vya wanafunzi kwa kuhudumia jamii.
Waziri amesisitiza juu ya umuhimu wa kuhimiza vijana wa Misri kushirikia mashindano yote ya kimataifa kwa sababu huwa na faida kadhaa na faida ya kwanza ni vijana watakuwa mabalozi bora zaidi kwa Misri wakati wa ushiriki wao wa kimataifa katika shughuli zote,kiasi kwamba wizara imeelekea kusanya mashindano yote ya kimataifa ya vijana katika orodha na kutosheleza kwa vijana wamisri ili kushiriki mnamo kipindi hiki.
Waziri ametoa amri kwa waafisa wa wizara kwamba inapaswa kuwa na mshikamano na ushirikano kati ya wizara na mpango wa wanafunzi wa Al_Azhar katika mradi wao,na kutafuta njia za ushirikiano na taasisi ya Inics Misri kwa ajili ya kutayarisha tartibu za kusaini kurasa ya maelewano na taasisi ili kudhamini uvumbuzi wa kielimu na kuhimiza miradhi ya vijana.
Taasisi ya Inakits, ni Shirika lisilolenga pesa au faida,kiasi kwamba linapatikana katika nchi 37 na linajumuisha vyuo vikuu 1730 ulimwengu, na linalenga kupunguza pengo kati ya elimu na soko la ajira kupitia wanafunzi wa vyuo vikuu wanatekeleza miradi inaweza kusuluhisha migogoro ya jamii na yanakuwa yana umbali wa kiuchumi, kijamii na kimazingira,na inawezesha wanafunzi kupata ujuzi, Ujasiriamali, mawasiliano na kufanya kazi pamoja na timu na kupata uwezo wa kuonesha , taasisi hii imeanzishwa mwaka 2004 ndani ya vyuo vikuu 4 na wanafunzi wa kiume na kike 120, leo inapatikana ndani ya vyuo vikuu 53 vya serikali na binafsi.
Na mwishoni Waziri Ashraf Sobhy ametoa vyeti kwa waliofuzu katika shindano la kimataifa kwa kuhuduma jamii 2020 : Sherif Sayed Mostafa , Yehia Mohamed Mohamed El Ghonemy ,Karim Gamal Nagy ,Eman Shawky,Ahmed Khaled,Nabil Esam Nabil,Ahmed Abd Elsalam,Sief Aldhin Nabil,Sara Elawadhy,Nadin Khaled,Huda Amer,Jana Ahmed, na Fatma Siri Mkuu wa programu ya Inakts,na Mohamed Alansary Mkurugenzi wa Programu.
Comments