Waziri wa Vijana na Michezo ahudhuria maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani Duniani huko Ismailia
- 2020-09-22 00:05:15
Jumatatu, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, ameshiriki katika maadhimisho yaliyofanyika mkoani mwa Ismailia ndani ya muktadha wa maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani ndani ya maadhimisho ya Siku ya Amani ya Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 21 ya kila mwaka ili kuimarisha maadili ya juu ya Amani kati ya watu na mataifa yote.
Maadhimisho yalihudhuriwa na Jenerali Sherif Beshara, Gavana wa mkoa wa Ismailia, Meja Jenerali Osama Rabie, Mkuu wa mamlaka ya mfereji wa Suez, Nahodha Walaa Hafez, Sameh El-Shazly, Rais wa Shirikisho la Misri kwa kupiga mbizi na kuokoa na kampuni ziandaazo.
Maadhimisho hayo yalishuhudia kuwekwa kwa alama kubwa zaidi ya Amani na koti za maisha 501 kama namba mpya imeyoonyeshwa kwenye Elezo la Ulimwengu la Guinness kwa usajili, kwa hivyo kwa kuzingatia kujitolea hatua zote za tahadhari na kinga zilizotangazwa na Wizara ya Afya Duniani kuzuia virusi vipya vya Corona.
Katika hotuba yake, Waziri huyo alielezea shukrani zake kwa washiriki wote katika maadhimisho ya Amani katika jiji la Ismailia, katika tukio la umuhimu la kueneza Amani, Ndugu, Upendo, kukataa Vurugu na Msimamo mkali.
Dokta Ashraf Sobhy aliashiria mwenendo wa serikali ya Misri wa kupanuka Amani na Upendo kati ya wote kwa kuzingatia sera bora ya Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, mwelekeo wa kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi ndugu zote na kutoa msaada kwa ujenzi na maendeleo.
Waziri huyo alitangaza msaada wa Wizara hiyo kwa mbizi mrefu zaidi na kukaa chini ya maji, kutekelezwa huko Sharm El-Sheikh kuvunja rekodi ya dunia, mapema Oktoba kama sehemu ya sherehe za kukumbuka ushindi wa Oktoba na ushiriki wa Nahodha Walaa Hafez.
Wakati Nahodha Walaa Hafez alisisitiza umuhimu wa kuimarisha maadili na desturi za kibinadamu, Amani na Uzalendo, na uwekezaji wa michezo katika kufikia misingi muhimu kama hiyo katika maisha ya mwanadamu, akitoa shukurani kwa pande zote zilizoshiriki kuandaa maadhimisho ya michezo katika ujumbe unaopelekwa na Misri kwa ulimwengu kwa kueneza Amani na Upendo kati ya mataifa.
Comments