Wadi Degla yaandaa mashindano ya CIB ya kimataifa kwa Boga kwa mwaka wa pili mfululizo


Klabu ya Wadi Degla ilitangaza kuandaa mashindano ya CIB ya kimataifa kwa Boga (2020),kwa mwaka wa pili mfululizo, katika kipindi cha 28 Septemba hii hadi 3 Oktoba ijayo, katika eneo la (The Park) kwenye duka la kiarabu linayohusiana na kampuni ya Vituo vya uwekezaji wa mali, mashindano haya yanajumuisha wachezaji 16 wazuri bora zaidi wa Boga ( wachezaji wa kiume 8 wazuri na wachezaji wa Kike 8 wazuri) katika uainishaji wa ulimwengu.


Miongoni mwa washindani kuna mashujaa watatu kutoka klabu za Wadi Degla wanashiriki katika mashindano haya, nao ni Nouran Johar aliyepata nafasi ya kwanza duniani, Ali Farag aliyepata nafasi ya pili duniani, na pia Kareem Abdul-Jawad aliyepata nafasi ya tatu.  


Mkurugenzi wa sekta ya Boga katika klabu za Wadi Degla "Kareem Darwish" amesisitiza " vikundi vya Wadi Degla vinatia juhudi za kuandaa washindani wanaoweza kushiriki katika maendeleo ya michezo ya kimisri na kushinda katika viwango vya kitaifa na kimataifa, na kupata lakabu zote katika mashindano ya kimataifa. Chuo cha Boga cha Wadi Degla, na ambacho ni chuo kikubwa cha Boga  ulimwenguni na kinajumuisha wachezaji 2500 kutoka wanachama wa klabu, kinasisitiza ushindi wa washindani wake, pamoja na klabu inaandaa mashindano ya kimataifa yaliyoingia kwenye Ajenda ya shirikisho la wachezaji wataalamu, na hiyo ni sawa na mtazamo wetu kwa ajili ya kugundua washindani wazuri ili wawe washindani wa siku zijazo.


Mashindano haya yana umuhimu kwani moja ya mashindano ya platinamu kulingana na Uainishaji wa shirikisho la kimataifa, kiwango cha zawadi zake za pesa kinafikia dola elfu 372 ili kugawanya sawa kati ya wanaume na wanawake, wachezaji wa kiume 8 bora zaidi katika kiwango cha ulimwengu kwa wanaume na wachezaji wa Kike 8 bora zaidi katika kiwango cha wanawake  wanashiriki katika mashindano hayo. 

Comments