Waziri wa michezo azungumzia nafasi za uwekezaji za kuanzisha tawi la "Klabu ya El Nady" na miradi ya taasisi ya Uwanja wa Kairo


Waziri wa vijana na michezo "Dokta Ashraf Sobhy alikutana na maafisa wa kundi la uwekezaji wa michezo ya Ghuba kwa kujadili ushiriki wao katika kuanzisha miradi kadhaa ya uwekezaji ndani ya shirika la uwanja wa Kairo . 

Maafisa wa uwekezaji wa michezo ya Ghuba Walionesha mawazo wazi kuhusu uwekezaji katika kuanzisha tawi la klabu ya El Nady na miradi ya Shirika la uwanja wa Kairo na kuanzisha majengo kadhaa ya uwekezaji karibu na uwanja huo.


Onyesho hilo limejumuisha  miundo ya ujenzi itakayojumishwa na tawi la klabu ya El Nady huko  uwanja wa Kairo , pamoja na jengo la Boga, jengo la klabu ya afya, hoteli ya michezo, eneo la viwanja vya kimataifa vya Tenisi, jengo la huduma, jengo la kuogelea, eneo la kucheza la watoto, jengo la kijamii, eneo la viwanja wa waanzilishi wa klabu, na maduka.


Hayo yote yanakuja  ndani ya mikutano kadhaa iliyofanywa na Waziri huyo pamoja na wawekezaji  kadhaa kwa kujadili ushiriki wao katika kuanzisha miradi kadhaa ya uwekezaji ndani ya Shirika la uwanja wa Kairo . Kwa ajili ya kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri, "Rais Abd El Fatah El-Sisi" Kwa kuruhusu matumizi ya jamii kwa Shirika la uwanja wa Kairo na majengo ya michezo yatayotekeleza baada ya ukarabati wake , na kuongeza ufanisi wake.


Waziri huyo aliomba kutoka kundi la uwekezaji wa michezo ya Ghuba kwa ajili ya kutoa taswira kamili kwa kuanzisha tawi la klabu ya El Nady  huko Shirika la uwanja na miradi ya uwekezaji inayopendekezwa kuanzishwa karibu na uwanja huo.inapaswa mradi huo unajumuisha kipindi maalum cha utekelezaji wa miradi na ukubwa wa uwekezaji wake kwa maandalizi ya kuangalia onyesho hili lililotolewa kutoka pande zake zote. 


Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza mfumo wa Wizara katika kuhimiza uwekezaji ndani ya majengo ya vijana na michezo  katika mikoa yote ya Jamhuri Kwa ushirikiano na sekta binafsi ndani ya mpango wa kutoa uwekezaji  kulingana na kanuni na sheria


zinazoongoza suala hilo.

Comments