Waziri wa Michezo akagua Kijiji cha Olimpiki katika Chuo Kikuu cha Assiut


 Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy, alitembelea Kijiji cha Olimpiki katika Chuo Kikuu cha Assiut, akifuatana na Meja Jenerali Essam Saad, Gavana wa Assiut, Dokta Tariq El-Gamal, Mkurugenzi wa Chuo Kikuu, na viongozi wa Wizara, Mkoa na Chuo Kikuu.


 Wakati wa ukaguzi wake wa Klabu ya Jamii na mkusanyiko wa kuogelea katika Kijiji cha Olimpiki, Sobhy alisifu kiwango bora cha washiriki katika mafunzo ya kuogelea na maendeleo ya ujenzi ndani yake, akisisitiza mapinduzi ya ujenzi katika vituo vya vijana na michezo huko Assiut na mikoa ya Juu ya Misri kwa jumla, ambayo ina sehemu kubwa ya mpango wa maendeleo wa serikali.


 Pembezoni mwa ziara hiyo, Waziri huyo aliwaheshimu washindi wa mbio za marathon zilizofanyika asubuhi ya leo, kwa ushiriki wa vijana na wasichana  wa Assiut, na kubadilishana ngao za kumbukumbu kati ya Waziri, Gavana wa Assiut, na Mkurugenzi wa chuo kikuu.


 Mahmoud Ashraf Ali alishika nafasi ya kwanza , ambapo Amr Hussein akishika ya pili ,   Bilal Khaled akishika nafasi ya tatu, Salah Ashraf akishika ya nne,  Ibn al-Walid Khaled akishika ya tano,  Mustafa Muhammad akishika ya sita,  Mustafa Hassan akishika ya saba,  Assem Hijab akishika ya nane,   Khaled Abdel Nasser  akishika ya tisa, na Ihab al-Din Mustafa akishika nafasi ya kumi.

Comments