Waziri wa michezo na Gavana wa Assiut waongoza mbio za Baiskeli katika barabara za Assuit


Mnamo asubuhi ya Jumamosi, Tamasha la Baiskeli lilianza chini ya alama ya "Mchezo wake ni Kinga yako"  likiongozwa na Dokta Ashraf Sobhy , Waziri wa Vijana na Michezo, Jenerali Essam Saeed Gavana wa mkoa wa Assiut  na Viongozi wa mkoa wa  kiutendaji, kisheria, na kienyeji, na japo la viongozi wa Wizara.


 Beji ya kuanza Tamasha  ilizinduliwa mbele ya diwani ya mkoa hadi kijiji cha Olimpiki kwenye Chuo kikuu cha Assuit na ushiriki wa kundi la Vijana na Wasichana wanaoendesha Baiskeli 100.


Dokta Ashraf Sobhy aliashiria kuwa kufanya Tamasha la Baiskeli, chini ya alama ya "Mchezo wako ni Kinga yako"mara kwa mara katika mikoa tofauti kunakuja katika shime ya nchi na uongozi wa kisiasa, kuufanya Mchezo uwe mtindo wa maisha, lililoanza kuhamasisha raia kufanya michezo kupitia Baiskeli, na Rais Abd, El-Fatah El-Sisi akiwaomba wamisri kutumia Baiskeli. 


Sobhy ameongeza kwamba "mpango wa Baiskeli yako ni Afya yako" uliozinduliwa na Wizara  ya Vijana na Michezo kwa kuzingatia maoni na maagizo ya uongozi wa kisiasa umepata kukubalika na idhini kubwa katika barabara ya Misri,

kati ya raia wote hasa Vijana.


 Akiashiria kuwa hatua ya kwanza na ya pili ya  kununua Baiskeli imekamilika, na hatua ya tatu inaandaliwa  kwa idadi kubwa kwa mikoa mbalimbali. 


Jenerali Essam Saad Gavana wa mkoa wa Assuit, alieleza furaha yake kubwa kwa ziara ya Dokta Ashraf Sobhy, na ufunguzi wa vituo vya Vijana na Michezo katika mkoa na kusisitiza juu ya kutulia kwa uongozi wa kisiasa, kwa watu wa Misri ya juu.


Jenerali Essam Saad Gavana wa mkoa wa Assuit alikuwa amempokea asubuhi ya Leo Do Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, kwenye ofisi yake katika diwani kuu ya mkoa, wakati wa ziara yake kwa mkoa ili kutoa Beji ya kuanza mbio za Tamasha la Baiskeli na kufunguliwa idadi ya vituo vya Vijana na Michezo  mkoani. 

Comments