Waziri mkuu aangalia mafanikio na maendeleo ya mkusanyiko wa kumbi zinazofunikwa kwenye uwanja wa Kairo kujiandaa mashindano ya kombe la dunia la mpira wa mikono


 Dokta Mostafa Madbuly Waziri mkuu wa Misri ameangalia mafanikio ya maendeleo katika mkusanyiko wa kumbi zinazofunikwa katika Uwanja wa Kairo,na hii ni moja wapo wa taratibu za kukaribisha mashindano ya kombe la dunia kwa mpira wa mikono yatakayoanza nchini Misri kuanzia Januari 13 hadi 31 2021, akiambatana na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo,  Dokta Hassan Mostafa, Mwenyekiti wa shirikisho la kimataifa kwa mpira wa mikono, Dokta Hisham Nasr, Mwenyekiti wa shirikisho la kimisri kwa mpira wa mikono, Jenerali Ali Darwish, Mwenyekiti wa shirika la Uwanja wa Kairo na kama mwakilishi wa shirika la uhandisi la jeshi ya Misri.


 Waziri mkuu akisifu kiwango cha ubora wa juu na kutengeneza kazi kwa kiasi kikamilifu kwa matendo ya kutayari kwa kukaribisha mashindano ya kombe hilo,katika Uwanja wa Kairo na  majengo mengine ya kimichezo  yatakayokaribisha kombe hilo,na akisisitiza  uwezo wa Misri kwa kukaribisha tukio hili la kimichezo kama inavyotarajiwa, na kutosheleza taratibu zote zinazohitajika ili kufanikisha tukio hilo.


Pia amefuatilia zote zinazohusiana na maendeleo ya kumbi zinazofunikwa katika Uwanja wa Kairo wa kimataifa,na amesikiliza maelezo ya programu ya kuendelea na uratibu wa programu ile,kiasi kwamba imepangwa kuwa ukumbi mkuu uliofunikwa huko Uwanja wa Kairo, wa uwezo wa mashabiki elfu 22 utashuhudia mechi za kundi la Misri.


 Wazir huyo ameeleza kwamba kazi za kuendelea kwa kiasi kikamilifu na kiwango kikubwa na inatarajiwa kazi hii itamaliza mwishoni mwa Oktoba ijayo,akiashiria kuwa kazi za maendeleo hujumuisha kuongeza ufanisi wa ukumbi mkuu,sakafu za ukumbi, vyumba vya mavazi,njia za kuingia za mashabiki na wachezaji,mifumo ya sauti na mwanga,mifumo ya idhaa ya ndani na ufasiri wa moja kwa moja pamoja na kujenga kituo  kipya cha habari na kituo cha mikutano ya habari kwa kuhudumia wanahabari na wawakilishi wa wakala za habari.


Vilevile ameonesha matayarisho ya kukaribisha wageni wa Misri kama wachezaji,makocha,maafisa na mashabiki katika kumbi zilizachguliwa kukaribisha michuano,na jukumu la watu walijitoa kwa kufanikisha hilo ,pia amesisitiza  jukumu muhimu la nchi la kurahisisha mizozo na shida zinazoukabili  upangaji wa  mashindano muhimu hayo  ya kimataifa . 

Comments