Waziri wa michezo akagua mazoezi ya kwanza ya " Out Door" ndani ya mpango wa " uwe mwanariadha " katika mji wa Nasr
- 2020-10-03 16:09:37
Jumanne asubuhi, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikagua " mazoezi ya wazi ya kwanza " katika bustani ya watoto huko mji wa Nasr kama sehemu ya mpango wa " uwe mwanariadha - Be Fit " ulioandaliwa na shirikisho la Misri kwa " workout street - sport street " kwa mahudhurio ya Rais wa Shirikisho Islam Kartam na japo la wataalam wa vyombo vya habari.
Hiyo inakuja ndani ya muktadha wa sera ya Wizara ya vijana na michezo na shirikisho la workout street la kuanzisha " mazoezi ya wazi " katika bustani na viwanja vya umma na kuandaa sherehe za michezo kwa mazoezi ya mwili mitaani.
Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza jaribio la uenezi wa utamaduni wa mazoezi ya michezo ndani ya jamii na kuifanya iwe njia ya maisha. Katika utekelezaji wa mkakati wa Wizara ya vijana na michezo kwa kuzingatia maagizo ya Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kuhamasisha raia kufanya mazoezi ya michezo kwa majukumu yake mengi mazuri juu ya afya ya raia.
Waziri huyo ameongeza, " tunatumia njia zote zinazowezekana na kupitisha mipango inayolenga uenezi wa michezo. Wizara hiyo inasambaza mashirikisho yenye ubora ili kufikia malengo yake, pamoja na shirikisho la workout street ili kueneza michezo kati ya raia ndani ya muktadha wa kuendeleza maendeleo ya michezo, kufanya kazi ya kuanzisha ukumbi wa michezo katika bustani na bustani za umma zikiwa na vifaa vya michezo kutoka kwa tasnia ya kimisri, na kampuni ya " Al-Modon " iliyoanzishwa na Wizara inahifadhi vifaa vilivyotolewa na kumbi hizi kuzihifadhi na kuhakikisha mwendelezo wake.
Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza utoaji wa sababu za usalama katika kumbi za michezo katika bustani zikiwa na vifaa vya mazoezi na vifaa vya michezo ya workout street, pamoja na kutoa makocha pamoja nao kuongeza viwango vya usawa wa raia kupitia mazoezi ya michezo, ikionesha kwamba mpango huo utasambazwa katika mikka anuwai kulingana na viwango vilivyowekwa katika suala hilo.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la workout street alisema : " tunatoa mfano na njia mbadala kwa vijana kufaidika na nguvu zao kwa kufanya mazoezi ya michezo katika viwanja vya bustani na Mibuga, tukitoa Shukrani kwa Waziri wa Vijana na Michezo kwa msaada wa kudumu uliotolewa na shirikisho.
Ikumbukwe kuwa Wizara ya vijana na michezo na shirikisho la workout street zimeweka maeneo kadhaa, viwanja na Mbuga za umma kwa ushirikiano na Wizara ya maendeleo ya mitaa na mikoa ya Kairo, Aleskandaria na Aswan kwa utekelezaji wa mpango huo, ambapo bustani ya uhuru imetambuliwa katika zamalek, bustani za Mei 15 na bustani ya Al-Azhar huko Kairo na katika mkoa wa Aleskandaria, mpango huo utatekelezwa katika sehemu ya Bir Masoud katika kitongoji cha Montazah, bustani ya Laurent, sehemu ya bustani Bayram Al-Tunisi katika eneo la Shatby , bustani ya Askari isiyojulikana huko Al- Manshiyya, katika mkoa wa Aswan hifadhi ya bustani ya hoteli ya Sheraton, inayojulikana na eneo lake moja kwa moja kwenye Mto Nile, ikiainishwa.
Comments