Timu ya taifa ya Morocco inajiunga mashindano ya mpira wa mikono kwa wanaume katika toleo la 27 nchini Misri 2021 baada ya kupoteza kwa miaka 14 mbali na matokeo ya kimataifa, baada ya Morocco imeshika nafasi ya sita katika mashindano ya kombe la nchi za Afrika nchini Tunisia 2020 , na imekuwa miongoni mwa timu za taifa sita katika mashindano hayo.
Morocco imeshiriki kwa mara sita katika mashindano ya kombe la dunia mwanzoni mwa mashindano ya 1995 katika Iceland na Muonekano wa mwisho umekuwa katika mashindano ya 2007 nchini Ujerumani, na mafanikio bora zaidi kwa masimba wa bahari kuu ya Atlantic katika mashindano ya Ufaransa mwaka 2001 na huweza kupata nafasi ya 17.
Kocha Nour Elden Bouhdioui huongoza Morocco aliyeweza kufanya mafanikio mazuri katika mashindano ya kombe la nchi za kiafrika na kombe la dunia, vilevile amekuwa kuongoza timu katika mashindano ya dunia , na anahangaika kuonesha timu katika hali nzuri baada ya kurudi kwa shughuli za kimataifa baada ya kupoteza kwa miaka 14.
Na Nour Eldin alisisitiza akisema: kazi yetu katika mashindano ya 2021 si rahisi kamwe haswa baada ya mripuko wa Janga la Corona, kiasi kwamba wachezaji wote wamesimamisha kucheza michezo kwa muda mrefu, sasa tumeanza kurejesha mazoezi na wachezaji wa ndani na kuweka programu kwa kutayarisha wachezaji kwa mashindano ya kombe la dunia.
Vilevile amesema:timu ya Morocco imeweza kurudia mashindano ya dunia baada ya kupoteza kwa miaka14, na namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba nimekuwa msimamizi wa timu katika mashindano yote iliyoyashiriki.
Na kuhusu mawazo yake ya timu katika awamu hii ya kisasa,kocha amesema:wakati huu ni wa kurekebisha na kufanya upya timu ya vijana inayoweza kuonesha imara yake katika mashindano ya kiafrika na kiarabu.
Kocha wa Morocco kuhusu kura ya michuano iliyosababisha kuwepo kwao katika kundi la sita pamoja na Iceland,Ureno na Algeria alizungumzia akisema: Naona kura hiyo ni nzuri, ambapo ni michuano ya Dunia siyo barani, inatakiwa kupambana timu kadhaa zinazo imara kama Iceland , Ureno na kuna timu kiwango chake cha umahiri na ustadi kikaribia au kushabihi ustadi wetu kama Timu ya Algeria ya kindugu na mechi itakuwa muhimu zaidi kwetu, kulingana na ukaribu katika umahiri.
Bouhdioui ana mpango imara katika mashindano kiasi kwamba amesema: nitategemea wachezaji ambao huchezea nje na wachezaji wa klabu za ndani na matumani yangu kufikia mzunguko wa pili.
Kocha wa Morocco ameandaa mpango kabla ya miezi kadhaa kabla ya kuyatangaza mashindano na amesisitiza: programu ya kuandaa ni muhimu zaidi tumeanza kuandaa katika Morocco halafu tutasafiri kuelekea Ufaransa na kurudi mara tena kwa Morocco halafu Ureno na safari ya mwisho itakuwa nchini Misri.
Comments