Waziri wa michezo akutana na kamati iandaayo kombe la mpira wa mikono la Dunia la 2021


Jumapili asubuhi, Oktoba 4, Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy, alikutana katika ofisi kuu ya Wizara ya vijana na michezo pamoja na kamati iandaayo kombe la mashindano la 27 la mpira wa mikono la Dunia, litakalofanyika nchini Misri , mapema ya 2021,  ushiriki wa timu 32, na mahudhurio ya Mhandisi Hisham Nasr, Rais wa Shirikisho la mpira wa mikono la Misri na mwenyekiti wa kamati iandaayo, kocha Hussein Labib ni mkurugenzi wa mashindano hayo, Dokta Ashraf Al-Sheikh ni mkurugenzi mtendaji wa Baraza la michezo la kitaifa, Rais wa kamati ya mawasiliano ya serikali katika mashindano hayo na viongozi wengine wa Wizara ya vijana na michezo.


Mkutano ulijadili maadalizi ya hoteli za malazi kwa timu na ujumbe ulioshiriki kwenye mashindano, pamoja na mpango wa matibabu wa mashindano na vifaa vyake kwa hatua za kinga ya virusi vipya vya Corona, Covid-19, inahitajika nini kwa uchambuzi na taratibu za hafla na ujumbe kabla ya kuja Misri, na taratibu na maagizo maalum wakati wa mashindano.


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri huyo, alithibitisha kuwa nchi ya Misri, likiongozwa na Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, linatoa msaada kamili na mahitaji yote muhimu kufanikiwa mashindano hayo, ambayo ni makubwa zaidi na ushiriki wa timu 32 kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo.

 

Wakati wa mkutano huo, Sobhy alisisitiza hitaji la kamati zote zinazohusika na mashindano kumaliza maadalizi yote kwao kwa muda maalum.


 Hiyo ilikuja wakati wa mkutano wa kila wiki, unaofanyikwa na Waziri wa Vijana na Michezo pamoja na kamati iandaayo kufuatilia maandalizi yote ya mashindano hayo.


Kwa upande wake, Mhandisi Hisham Nasr alimshukuru Waziri wa Vijana na Michezo kwa juhudi zake bila kuchoka katika kurahisisha vizuizi vyote vinavyoikabili kamati iandaayo na nia yake ya kutekeleza kazi zote kulingana na viwango vya kimataifa.


Ikumbukwe kuwa timu ya kitaifa ya mpira wa mikono ilichagua kucheza katika kundi la saba katika mashindano ya ubingwa na Uswidi, Jamhuri ya Czech na mwakilishi wa Marekani Kusini wakati wa kura iliyofanyikwa kwenye Piramidi huko Giza. 


Comments