Waziri wa michezo atoa mpango wa "Misri bila washukwa majini" ili kuwaelimisha wananchi kwa stadi za kuokoa
- 2020-10-11 12:13:01
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo, katika mkutano mkubwa zaidi wa habari uliokaribishwa kwa jukwaa la Wizara, Jumatatu 5/10 , alitoa shughuli za mpango wa "Misri bila washukwa majini" kuongeza ufahamu, na kueneza utamaduni wa kuokoa kwa mwananchi kwa lengo la kupunguza misiba ya kuzama.
Shughuli za mkutano huo zilihudhuriwa na Kapteni "Sameh El Shazly" Msimamizi wa mashirikisho mawili ya Misri na ya kiarabu kwa kupiga mbizi na kuokoa, na Dokta Mohammed Saleh Naibu wa Rais wa Shirikisho la kuokoa la kimataifa, na Dokta Hisham Al Jayoushi, sekretarieti wa Shirikisho la michezo la vyuo vikuu, Nahodha Walaa Hafez, na Dokta Hazem Al Ruby Mratibu wa mpango, na idadi kadhaa ya viongozi wa Wizara.
Mpango unalenga kuwaelimisha na kuwapatanisha wakombozi wanaofanya kazi kwenye fukwe tofauti, na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vilivyohitajika vya bima ya pwani na bahari, na kufanyika semina na mikutano kuelimisha raia na kumfundisha kwa uzoefu msingi wa kuokoa katika mikoa tofauti.
Mkutano ulijumuisha kuonesha ripoti yenye picha kuzunguka rekodi mpya ulimwenguni iliyosajiliwa kwa jina la Misri katika Elezo la Guinness la Rekodi la ulimwenguni kupitia kuunda neno kubwa zaidi la Amani (Peace) kwa makoti ya kuokoa 501 katika wakati wa rekodi kwenye kingo za mfereji wa Suez jijini mwa Ismailia miongoni mwa sherehe za siku ya Amani duniani, pamoja na kuonesha filamu fupi kuhusu shughuli kuu zaidi zilizotekelezwa na Shirikisho la kupiga mbizi na kuokoa la Misri, na maonesho kuhusu maoni, ujumbe na vifaa vya kutekeleza mpango wa "Misri bila washukwa majini", na taratibu za bima ya bahari.
Na katika hotuba yake, Dokta Ashraf Sobhy, alisema : "Mpango wa Misri bila washukwa majini kuwaelimisha na kuboresha uzoefu wa vijana na wananchi katika uzoefu wa kuokoa unakuja sambamba na mkakati wa ujenzi wa binadamu uliotolewa na Rais Abd El Fatah El Sisi, Rais wa Jamhuri," akizungumzia msaada wa Wizara kwa mpango kwa umuhimu wake ndani ya jamii.
Waziri wa vijana na michezo alisisitiza kuungana kwa wote na kuratibu na mamlaka husika kwa ajili ya kutekeleza na kuhakikisha malengo ya mpango huo na kutia ndani uendelevu wa kazi, akitoa shukrani kwa Shirikisho la Misri na mashirikisho ya kimataifa na ya kiafrika ya kupiga mbizi na kuokoa kwenye hatua muhimu, pia jitihada zilizofanywa wakati uliopita, na kupasha Misri rekodi ya ulimwenguni kupitia sherehe za siku ya Amani duniani huko mkoa wa Ismailia.
Kwa upande wake, Sameh Al Shazly alieleza kuwa wazo la " Misri bila washukwa majini" lilikuja baada ya ajali mbaya iliyotokea katika pwani ya Al Nakhel na karibu watu 12 walizama, akiashiria kuwa mpango unategemea pande kadhaa, wa kwanza kwa kushirikiana na Shirikisho la kuogelea la Misri, nayo ni kuondoa kutofahamu kwa kuogelea kwa wanafunzi wa shule, na wa pili kwa wanafunzi wa vyuo vikuu ambapo kuingizwa kwa somo la kuokoa kama somo la kimsingi katika vitivo vya elimu ya riadha na kuwaelimisha wanafunzi wa vitivo tofauti, upande wa tatu unategemea kuwaelimisha wananchi ndani ya vituo vya vijana na vilabu vya michezo katika mikoa yote, na kufanya semina, mikutano na vipindi vya mazoezi.
Msimamizi wa Shirikisho la kuzama na kuokoa aliomba kulazimisha Shirikisho kwa Usimamizi wa kiufundi juu ya kuokoa katika bahari zote, vijiji vya utalii na hoteli, akitoa shukrani na kutathmini kwa Waziri wa vijana na michezo kwa utunzaji wake kwa mpango huo.
Ambapo Naibu wa Rais wa Shirikisho la kuokoa la kimataifa alionesha shughuli za Shirikisho la kimataifa kwa kutekeleza hatua ndani ya barani Afrika kupunguza ajali za washukwa majini, akiashiria kuwa Misri imechukua hatua ndani ya bara kwa kutekeleza mpango wa "Misri bila washukwa majini", akizungumzia kutoa uzoefu wote wa kimataifa katika jambo hili kuhakikisha hatua ya Misri kwa lengo kuu la hatua kwa kufikia Misri bila washukwa majini mwaka wa 2025.
Mkutano ulishuhudia kutoa alama ya reli
#Misri_bila_washukwa majini kwenye mitandao ya kijamii chini ya kauli mbiu ya "Maisha yako ni yenye thamani .. tunayatunza"
Comments