Waziri wa michezo : Subirini Mashindano ya dunia ya Kinjia ya wachipukizi nchini Misri Aprili 2021
- 2020-10-11 12:16:53
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo, alikutana na Dokta Wajih Azzam, Mkuu wa shirikisho la Baiskeli la Misri, kutafutia matayarisho kwa ajili ya kukaribisha mashindano ya Dunia ya Kinjia ya wachipukizi nchini Misri Aprili 2021, kwa mahudhurio ya Elec Lenferna, Mkurugenzi wa mashindano, Mohammed Al kurdi, Msaidizi wa Waziri , Dokta Abdul Awal Mohammed, Naibu wa Waziri katika sekta ya mashindano.
Waziri huyo, alisisitiza utunzaji wake kwa kuamsha na kutia moyo kwa kufanya mchezo wa Baiskeli katika maisha kwa jumla, akiongeza kuwa kuna mpango wa kuhakikisha hilo mnamo kipindi kijacho, akisisitiza kuwa Wizara hujaribu kuwa kufanya michezo kwa jumla na haswa Baiskeli kuwa mtindo wa maisha kwa wamisri.
"Sobhy" aliashiria kuwa kufanya michezo ni moja ya malengo muhimu zaidi ya nchi katika pande za michezo na afya na ina umuhimu mkubwa kwa vijana ambapo husababisha kwa watu wote kuwachochea kufanya michezo iliyotegemezwa daima na ilisisitizwa mara nyingi na Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El Sisi.
Rais wa Shirikisho la Baiskeli la Misri aliashiria kuwa, Shirikisho la Baiskeli liko tayari daima na katika wakati wowote kukaribisha na kuandaa mashindano yoyote ya kimataifa au duniani haswa baada ya mafanikio na kwa ushahidi wa watu wote duniani kote katika ubora wa Misri katika pande zote za kuandaa mashindano yote ya kimataifa yaliyopewa kwake mnamowakati uliopita, akitoa shukrani kwa Waziri wa vijana na michezo kwa juhudi zake na msaada wake wa daima kwa Shirikisho la Baiskeli la Misri.
Hilo linakuja miongoni mwa makubaliano yaliyofanyikwa na Waziri wa vijana na michezo pamoja na wakuu wa mabaraza ya idara ya mashirikisho ya michezo kufuata mpango wa kazi wa mashirikisho ya michezo, na kutafutia taratibu za mashindano ya kimataifa yatakafanyikwa nchini Misri mnamo kipindi kijacho.
Comments