Waziri wa vijana akutana na wawakilishi wa Shirika la UNICEF nchini Misri na akagua maonesho kwa bidhaa za mpango wa Mishwari
- 2020-10-13 11:23:12
Waziri wa vijana amewapokea Bwana Ted Shipan, Mkurugenzi wa eneo la kaskazini ya Afrika na Mashariki ya kati kwa Shirika la UNICEF na Bwana Germy Hopkanz, Mwakilishi wa Shirika nchini Misri kwa kutafutia njia za ushirikiano kati ya Wizara na Shirika hilo mnamo kipindi kijacho, kwa mahudhurio ya Jenerali Ismail Alfar , Rais wa Idara kuu ya miradi na kuwafundisha vijana na Bwana Ashraf Albgramy Mwakilishi wa Kurugenzi la Wizara ya vijana mjini Kairo.
Dokta Ashraf sobhy na wawakilishi wa UNICEF wamekagua maonesho ya bidhaa ya kiufundi kwa mpango wa Mishwari mjini Kairo na baada ya hivyo, kulikuwepo kuonesha mifano yenye ufanisi katika mpango huo unaotekelezwa na miradi kuwafundisha vijana kwenye Wizara pamoja na ushiriki wa shirika la Umoja wa mataifa kwa watoto (UNICEF) unaofundisha vijana kwa soko la ajira na kunukia umahiri wao wa maisha kwa wachipukizi na vijana.
Waziri wa vijana amesisitizia alipopokea ujumbe wa UNICEF kurahisiha kuweka mipango ya kimkakati kwa kuhakikisha malengo makuu ya programu akiashiria kwamba programu ya Mishwari lengo lake hukubalina na mipango ya kuendelea kuunda binadamu katika maisha uliozinduliwa na Rais Abd El Fatah El-Sisi katika mkutano wa vijana wa hivi karibuni pamoja na umuhimu wa kueneza vizuri kwa bidhaa ndani na nje, vilevile kutembelea maonesho ya Turathna (Urithi wetu) yanayojumuisha bidaa za mikono,matoleo ya kitaifa na kuonesha bidhaa ya kitaifa kwa ulimwengu.
Waziri ameonesha juhudi za nchi kwa kunukia uwezo na ustadi wa uongozi na usimamizi kutoka Chuo kikuu cha Aslska kwa kutoa nafasi kikubwa kwa vijana kwa kuwa katika nafasi ya kuongoza katika nchi, pamoja na mchango wa chuo cha kitaifa kwa kuimarisha vijana, vilevile ameonesha tartibu za Wizara kwa kuhimiza vijana na mibio yaliyofanikiwa katika mikoa kadhaa tofauti na kuhimiza wazo la uwezo wa kupundukia programu ya Mishwari kwa kuongoza miradhi pamoja na kuwepo kwa kampuni ya kitaifa inayohusiana na matoleo ya kiufundi.
Mkurugenzi Mkuu wa eneo wa Shirika la UNICEF ameashiria umuhimu wa mafanikio ya programu ya Mishwari chini ya uangalifu wa Wizara katika mikoa kumi na moja,
Akisifu umuhimu wa kukamilisha miradi na uwekezaji katika binadamu na kuhimiza binadamu.
Vijana wa Mishwari wameonesha kisa cha ufanisi wao tangu walipojiunga programu hiyo ambayo imefanikiwa katika mikoa ya Jamhuri na jinsi walivyojiunga na wamepata nini kutoka mpango huo.
Lengo la programu ya Mishwari ni kuendelea umahiri wa maisha kama mawasiliano na kuainisha malengo, kuwaza kiubunifu na umahiri wa kujiandika kama kuandika Tawasifu ,na kupitisha Usaili , kujenga miradi midogo kwa vijana pamoja na vituo vya kuhudumia kutoa ushauri kwa vijana.
Comments