"Vijana na Michezo" yaendelea shughuli za mradi wa kitaifa kugundua talanta za mpira wa Miguu

Wizara ya Vijana na Michezo inaendelea na shughuli za mradi wa kitaifa kwa wanasoka wenye talanta (Watu wenye talanta katika mpira wa miguu)  "Nyota wa Misri", unaotekelezwa nayo kwa  pamoja na kampuni ya Uholanzi, Star Lab, kampuni husika katika uwanja wa maendeleo ya michezo, na Chama cha kugundua kwa Talanta wa Kiingereza; Kugundua na kulea watu wenye talanta kutoka kwa mikoa tofauti ya Jamhuri, kulingana na kanuni na vipimo vya kisayansi.


Vijana 1100 mnamo kipindi  cha umri wa miaka 6 hadi 18 wamepitia mitihani iliyofanywa na idara  ya mradi katika Kituo cha Vijana cha Al Jazira, wakati wa miezi ya Januari na Machi mwaka huu, Ambapo vijana 200 wenye talanta bora zaidi walioanza mitihani  walichaguliwa, 11 kati yao walikuwa wachezaji waliodhaminiwa ambao walisainiwa, kwa sababu ya kufanikiwa kwao kwa kiwango cha juu zaidi kwenye majaribio, nao ni nyota 3. 


Wizara ya Vijana na Michezo inaandaa  mazoezi ya kila wiki kwa wachezaji wanaopata mazoezi katika Kituo cha Vijana cha Al-Jazira kama kituo cha kwanza kuandaa mazoezi  ya mradi huo,  yaliyoanza Julai iliyopita, na ushiriki wa wakufunzi maalum,  miongoni mwao ni  David Hobson, mwanzilishi mkuu wa Chama cha kugundua Talanta za Kiingereza, na David White House, Rais wa Chuo cha Junior katika Kilabu cha Manchester United, na  usimamizi  wa moja kwa moja kutoka Kocha Adel Abdel Rahman, mkurugenzi wa kiufundi wa Misri wa mradi huo.


Mradi wa kitaifa wa kugundua "Nyota wa Misri"  watu wenye talanta umepangwa kufikia mikoa mbalimbali  wakati wa  kipindi kijacho, kwani vituo 16 vya mradi vitaanzishwa katika vituo vya kijiografia vinavyohusu mikoa  yote, na wale wanaokuja kushiriki watachunguzwa mitihani  na vipimo vya kisaikolojia. ili Kujua talanta, ikifuatiwa na awamu ya mazoezi na ujuzi, na ushiriki utatangazwa katika kila mkoa tofauti kabla ya kuanza kwa mradi kwa wakati wa kutosha.


Katika muktadha huu, idara ya mradi ilitangaza kuendelea kwa vipimo katika Kituo cha Vijana cha Al Jazira.Wale wanaotaka kushiriki katika hiyo wanapaswa kununua fomu ya usajili inayopatikana katika Kituo cha Vijana cha Al Jazira, au kupitia kuingia kwenye tovuti ya mradi na kusajili data zinazohitajika www.starsofegypt.com


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na michezo , alielezea  kuwa mradi wa Nyota wa Misri unakuja katika fungu la miradi inayotekelezwa na Wizara. Kuchagua watu wenye talanta katika michezo tofauti , kuwapa msaada na kuwajali, na kuwaandaa vyema kama mabingwa wa siku zijazo, kwa maagizo ya Rais Abd El Fatah  El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kugundua watu wenye talanta na kueneza utamaduni wa mazoezi ya michezo ndani ya jamii.


Waziri huyo alisifu ushiriki wa wataalam wa kigeni na makocha katika shughuli za mradi wa "Nyota wa Misri", kwa kushirikiana na makocha maalum wa Misri,  inayochangia  kubadilishana uzoefu, na kuhakikisha uteuzi wa watu wenye talanta kulingana na viwango vya kimataifa katika mpira wa miguu. Inatarajiwa kwamba mradi huo utatoa nyota kwenye mchezo wa mpira wa miguu sawa na nyota wa timu ya kitaifa ya Misri na kilabu. Liverpool, timu ya Kiingereza, Mchezaji Mohamed Salah.


Kwa upande wake, Amr Muhanna, mkurugenzi wa mkoa wa Star Lab huko Misri,  ,Mashariki ya Kati na Afrika, na mkurugenzi wa mradi wa Nyota wa Misri, alithamini kiwango mashuhuri cha wachezaji wanaoshiriki katika mradi huo hadi sasa,  inayoahidi mustakabali mzuri kwao, ambao pia utaonekana katika maendeleo wa mpira wa miguu wa Misri, akisisitiza kuwa maandalizi na mazoezi  yanaendelea. Wacheza kila wiki kama sehemu ya utunzaji na msaada wanaopewa. 


Meneja wa mradi “Nyota wa Misri” alitangaza, katika kipindi cha sasa , kuwa uenezwji wa moja kwa moja wa wachezaji wenye kipaji (talanta) waliokuwa na ziadi miaka 16, kwa ajili ya utaalamu katika vilabu vya michezo. pamoja na maandalizi na mafunzo yanayotokea ya vijana 200 katika kituo cha “ vijana vya Al Jazira”, kulingana na kanuni za mafunzo  zilizowekwa na wataalam wa kigeni wanaoshiriki katika mradi huo. 


Ikumbukwe  kuwa usimamizi wa mradi wa kitaifa wa kugundua vipaji katika mpira wa miguu uliandaa tamasha la kwanza la kipaji cha mpira wa miguu chini ya utunzaji wa Waziri wa vijana na michezo  kama sehemu ya sherehe ya ushindi wa Oktoba, ambapo vijana  wachipukizi 200 walishiriki, ambao waligawanywa katika timu kadhaa ambazo zilishiriki mechi 20, na mwisho wa mechi wachezaji walipewa medali ya tamasha na kombe la timu ya kwanza. Na mchezaji bora kwa kila umri. 


Comments