Ali Farag apewa taji la ubingwa wa Misri wa kimataifa wa Boga na apate tena mwanzo wa uainishaji duniani
- 2020-10-18 23:03:43
Bingwa wa Misri Ali Farag aliyepata nafasi ya pili ulimwenguni katika ubingwa wa CIB wa Misri wa kimataifa wa Boga , uliopokelewa kwa Piramidi kama moja ya ubingwa mkubwa zaidi wa kipilatini katika Dunia ya Boga , ambayo ni ya juu zaidi katika mashindano ya mchezo , ambapo thamani ya zawadi za kifedha ni karibu dola elfu 270 kwa wanaume na hivyo ilivyo kwa wanawake , hiyo ilikuwa baada ya kumshinda Tarek Momen mwenye nafasi ya nne ulimwenguni.
Ali Farag alimshinda Tarek Momen kwa vipindi vitatu katika mechi iliyoendelea kwa dakika 38 , tokeo la mechi kama hivyo : 11_8,11_3,11_4.
Kwa tokeo hilo bingwa wa Misri alirejesha tena umbele wa uainishaji wa dunia, ambao aliupoteza mnamo Februari iliyopita , baada ya miezi tisa tu ya kutawala kwa Mohamed El_Shorbagy kuanzia Februari iliyopita mpaka Oktoba hii , ambapo Shorbagy hakushirki katika ubingwa wa kisasa .
Bingwa wa Misri Nour El_Sherbini alipewa jina la wanawake , akashinda kwa vipindi vitatu dhidi ya Noran Gohar aliyeainishwa katika nafasi ya kwanza ulimwenguni , katika mechi iliyoendelea kwa dakika 38 na tokeo la mechi lilikuwa : 11_9,11_9,11_6 .
Kwa tokeo hilo bingwa wa Misri aliweza kurejesha umbele wa uainishaji wa dunia wa Boga ambao aliupoteza mnamo Disemba mwaka 2018 , kwa bingwa aliyestaafu Ranem Elwali , wakati alipoaga ubingwa wa Hong Kong kutoka robo fainali , kabla ya kurejesha umbele baada ya miezi 23 mfululizo.
Tarek Momen alikuwa ameshamshinda Marawan El_Shorbagy aliyeainishwa katika nafasi ya saba duniani katika mechi ya nusu fainali kwa vipindi vitatu dhidi ya vipindi viwili katika mechi iliyoendelea kwa dakika 68 na tokeo la mechi lilikuwa :
5_11,11_6,11_3,11_13,11_6 .
Wakati ambapo Ali Farag, aliyeainishwa wa pili Duniani, alimalizia vituko vya ajabu dhidi Mustafa Al_Asal mchezaji wa Klabu ya Alahly na bingwa wa ulimwengu kwa vijana na aliyeainishwa katika nafasi ya 18 duniani , akamshinda kwa vipindi vitatu dhidi ya kipindi kimoja katika mechi iliyoendelea kwa dakika 71 na tokea lake lilikuwa : 11_3,11_7,12_14,11_4 .
Na katika mashindano ya wanawake , Nour El"Sherbeni alimshinda mwenzake Nour Eltayb aliyekuwa katika nafasi ya nne , Nouran Gohar akamshinda mwenzake Hanha Elhamamy mwenye nafasi ya saba .
Ikumbukwe kuwa Karim Abdel Gawad mchezaji wa klabu ya Wadi Degla mwenye nafasi ya tatu duniani na mwenye jina la ubingwa uliopita , hakushirki katika mashindano ya kisasa kuanzia mechi ya 32 kupitia mwenzake Mazin Hesham , japo bingwa wa Misri Nour Elsherbiny mwenye nafasi ya pili duniani alipewa jina la ubingwa uliopita wa wanawake.
Comments