Waziri wa Michezo ahudhuria sherehe ya kutoa tuzo za mashindano ya Boga ya kimataifa ya Misri kwa washindi


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia sherehe ya kutoa tuzo za mashindano ya Boga ya kimataifa ya Misri,ambapo mchezaji Ali Faraj aliposhinda lakabu ya ubingwa katika mashindano ya wanaume na mchezaji Nour El-Sherbiny alishinda lakabu ya ubingwa katika mashindano ya wanawake, kama sehemu ya shughuli za mashindano zilizoandaliwa na Misri kutoka 10-17 Oktoba kwenye uwanja wa glasi chini ya Piramidi na ushiriki wa wachezaji 96 kutoka nchi tofauti za ulimwengu.


Sherehe ya tuzo ilihudhuriwa na Dokta Khaled Al-Anani, Waziri wa utalii na mambo ya kale, Balozi Nabila Makram, Waziri wa uhamiaji na mambo ya wamisri nje ya nchi, Asim Khalifa, Rais wa Shirikisho la Boga la Misri, Amr Mansi, Mkurugenzi mtendaji wa mashindano hayo, wadhamini kadhaa na wasanii.


Mchezaji Ali Farag alimpiga mpinzani wake, Tarek Moamen katika mechi ya mwisho ya mashindano ya wanaume kwa matokeo ya seti tatu bure, wakati mchezaji Nour El-Sherbini alimshinda mchezaji Nuran Jahar katika fainali ya wanawake.


Waziri wa Vijana na Michezo aliwapongeza wachezaji kwa ubora wao katika uchezaji wa mechi na kufanikiwa kushinda lakabu la ubingwa katika kiwango cha mashindano ya wanaume na wanawake, akiwatakia mafanikio na wachezaji wote wa Misri na kuendelea kutoa utendaji bora wa hali katika mashindano tofauti ya kimataifa yaliyopangwa kwa ushiriki wao mnamo kipindi kijacho.


Waziri huyo alisifu juhudi zote zilizofanywa na kamati iandaayo  mashindano hayo, nia yao ya kuiondoa kwa njia bora na kufikia mafanikio ya hali ya juu, inayothibitisha ubora wa Misri katika kiwango cha kuandaa mashindano ya kimataifa, pamoja na nia ya kutumia viwango vya juu afya na usalama kwa uratibu na mamlaka inayojali kuzuia Virusi vipya vya Corona, alisifu eneo mashuhuri la akiolojia la Piramidi,ambapo  shughuli za ubingwa zilipofanyikwa.


Dokta Ashraf Sobhy alitangaza mashindano makubwa ya kimataifa ya michezo yatakayofanyika nchni Misri mnamo kipindi kijacho na mbele mashindano ya mpira wa mikono ulimwengu kwa wanaume mnamo Januari ijayo, akionyesha kuwa utunzaji wa mashindano haya ya Misri utakuwa na athari nzuri katika kiwango cha uchumi, kukuza utalii na uratibu kati ya utawala wa utalii wa michezo katika Wizara ya vijana na michezo na Wizara ya utalii na mambo ya kale katika suala hilo.


Ikumbukwe kuwa mashindano wazi ya kimataifa ya Boga  " wanaume na wanawake " ni moja ya mashindano 8 makubwa ya kimataifa ya plantinamu kwa wanawake na wanaume na wachezaji hushindania jumla ya tuzo hadi pesa elfu dola 540 ambayo ni jumla kubwa ya Boga ya tuzo kwa mashindano ya msimu huo.

Comments