Vijana na Michezo yajiandaa kutekeleza mashindano ya kwanza ya Wizara katika Soka na Tenisi ya meza

 Chini ya udhamini wa Dokta Mustafa Madbouly, Waziri Mkuu, kwa mara ya kwanza, Wizara ya Vijana na Michezo iliyoongozwa na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na kupitia Idara kuu ya Maendeleo ya Michezo na Shirikisho la Michezo kwa Wafanyikazi wa Serikali, ilitangaza kuanza kwa maandalizi yake ya utekelezaji wa mashindano ya Wizara katika  mpira wa miguu ya wanaume wa pande tano na Tenisi ya meza kwa wanawake, kwa  Wizara  na Ofisi Kuu ya Baraza la Mawaziri 33, mnamo Novemba ijayo katika moja ya vituo vya michezo na vijana vilivyoshirikiana na Wizara, kuchukua hatua zote za tahadhari na kinga kulingana na kanuni zilizotolewa na Wizara.

 

Waziri huyo, Dakta Ashraf Sobhy alisema kuwa wazo la ligi hiyo lilitokana na kujali kwa  Mheshimiwa Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa afya ya raia na kuwahamasisha kufanya mazoezi ya michezo kila siku, haswa vifaa vya utawala wa serikali, kuongeza uzalishaji, na kwa kuzingatia maoni na mkakati wa Wizara kuelekea kuifanya michezo kuwa njia ya maisha, na uwekezaji wa mafanikio ya tamasha la kimichezo la kwanza katika jiji jipya la El Alamein, ambapo Waziri Mkuu na Mawaziri kadhaa walishiriki.

Akisisitiza kuwa lengo la ligi hiyo ni kuunganisha  Wizara na kuhamasisha idadi kubwa ya wafanyikazi katika vifaa vya kiutawala kufanya mazoezi ya kila siku, kubadilisha mtindo wa maisha wa washiriki, kupanua msingi wa mazoezi ya michezo, kuboresha hali ya washiriki na kuboresha afya yao kwa jumla.


Mashindano ya Wizara, ambayo hufanyika kwa mara ya kwanza chini ya udhamini wa Waziri Mkuu, Wizara 33  pamoja na Ofisi Kuu ya Baraza la Mawaziri, zitashiriki katika michezo miwili ya mpira wa miguu wa wanaume wa pande tano na Tenisi ya meza ya wanawake, na ushiriki wa washiriki 510 kutoka timu 34 kwa kila mchezo, ikimaanisha washiriki 15 na kutoka kila Wizara  Wachezaji 8,  wawili wa akiba, msimamizi, Kocha wa Soka ya pande tano, na wachezaji 3 wa kike, msimamizi, na Kocha wa Tenisi ya meza.

Comments