Misri yaingia Elezo ya Guinness kwa kurekodi mchezaji mkubwa zaidi wa mpira wa miguu ulimwenguni
- 2020-10-23 18:53:35
Dokta Ashraf Sobhy: Mchezo wa Misri umepata mafanikio mfululizo ulimwenguni kwa msaada wa uongozi wa kisiasa.
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alitangaza kuwa Misri imepata rekodi mpya ya ulimwengu katika "Guinness World Records", kwa kusajili mchezaji mkubwa zaidi wa Misri katika mpira wa miguu ulimwenguni katika Elezo hilo "Mhandisi. Ezz El-Din Bahader," mwenye umri wa miaka 75 kama mchezaji mkongwe zaidi ulimwenguni baada ya Shirikisho la mpira wa miguu la Misri kumalizika taratibu za usajili wake Januari iliyopita, baada ya klabu ya Oktoba 6 kufanya mkataba wa nafasi ya tatu pamoja nayo.
Waziri wa Vijana na Michezo alipokeza cheti cha Rekodi za Ulimwengu za Guinness kwa mchezaji Ezz El Din Bahader baada ya rekodi katika ensaiklopidia baada ya ushiriki wake kwenye mchezo kati ya timu yake mbele ya klabu ya Al Ayat , iliyofanyika katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi kwa mahudhurio ya washiriki wa Kamati ya Miaka Mitano ya Usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu, Bodi ya Wakurugenzi ya washiriki wa klabu ya Oktoba 6 ,na wengi wa jamaa zake.
Waziri huyo alimpongeza mchezaji Ezz El Din Bahader kwa kufanikisha rekodi ya ulimwengu kwa kusajili katika Elezo la Guinness katika mafanikio mapya yatakayoongezwa kwenye mfumo wa michezo wa Misri kwa jumla na mpira wa miguu wa Misri haswa, akimtakia mafanikio na timu yake mnamo kipindi kijacho.
Dokta huyo alisisitiza kwamba mchezo wa Misri umetambulika ulimwenguni katika hafla anuwai za kimataifa, na uwasilishaji wa mabingwa wa Misri kwa onesho maarufu linalovutia kila mtu, na linaonesha kiwango cha maendeleo yaliyopata michezo ya Misri wakati wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, ambaye hutoa msaada kwa watu wa Misri katika nyanja tofauti.
Waziri huyo alisema kuwa Wizara inatoa msaada na utunzaji wote kwa wachezaji katika michezo tofauti, na msaada wao ili kufikia mafanikio ya Misri katika vikao anuwai vya kimataifa, akiashiria msaada uliotolewa na Wizara kwa mchezaji Ezz El-Din Bahader kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka na Klabu ya Oktoba 6 ili kumaliza mahitaji yote ya usajili wake Kama mchezaji mkongwe zaidi ulimwenguni katika Elezo la Guinness.
Waziri pia alibaini mafanikio ya hivi karibuni ya Misri katika kufikia rekodi ya ulimwengu katika Elezo la Guinness kwa kubuni neno la "Amani" na voti 501 za maisha katika mji wa Ismailia kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Amani Duniani kwa kuzingatia mafanikio mfululizo ya michezo ya Misri.
Sobhy alifunua kuwa michezo ya Misri inaishi kipindi kinachojaa mafanikio katika viwango tofauti kutokana na mshikamano wa sehemu zote za mfumo wa michezo, na hamu ya wachezaji kuheshimu Misri katika mashindano yote na kushinda, akionesha kwamba Wizara, Kamati ya Olimpiki na mashirikisho ya michezo wanafuata kwa karibu utayari wa wachezaji wa Misri kwa mashindano anuwai ya kimataifa. Na kutiwa moyo kushinda taji zao kulingana na mafanikio na mafanikio wanayo katika rekodi ya michezo ya Misri.
Comments