“Sobhy” na “Al Anani” watafutia kushirikiana katika uwanja wa utalii wa kimichezo
- 2020-10-23 18:56:44
Dokta Ashraf Sobhy –Waziri wa vijana na michezo- ameonana na Dokta Khaled Al Anani –Waziri wa utalii na mambo ya kale- ili kuzungumzia njia za kushirikiana baina ya Wizara mbili kwa kukuza bidhaa ya utalii wa kimichezo, na njia ya kupata faida kutoka matokeo ya kimichezo ya kimataifa na kitaifa kwa kukuza utalii wa kimisri, hivi kwa mahudhurio ya viongozi wa Wizara mbili.
Kwa upande wake, Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza umuhimu wa jukumu la wizara ya utalii na mambo ya kale kwa kutatua matatizo na vikwazo vyote vinavyokabiliana Wizara ya vijana na michezo wakati wa kufanya matokeo kadhaa ndani ya maeneo ya kihistoria. Akiashiria kuwa Wizara ya vijana na michezo inajaribu daima kupata ushirikiano na mashirika yote ya serikali kwa kuhuduma vijana wa Misri katika viwango vyote. Vijana wa Misri wana jukumu muhimu sana katika kujenga jamii, wana nishati kubwa zaidi, mawazo ya ubunifu katika nyanja zote, na wana shauku kwa kutatua matatizo na kukabiliana changamoto.
Waziri wa vijana na michezo aliashiria kuwa kuratibu na wizara ya utalii na mambo ya kale kazi ya kukuza nje kwa maeneo ya kihistoria ya kimisri itafanywa katika mashindano ya kimataifa yote ambayo mabingwa wa kimichezo watakayocheza; inayosisitiza kuwa Misri ni msingi wa ustaarabu na asili ya historia, na hiyo inapinga uvumi wowote wa uwongo unaotumiwa nje ya nchi, akionesha kuwa wizara ya vijana na michezo itaweka shughuli zote za michezo zijazo katika orodha ya Wizara ya utalii na mambo kale kwa ajili ya kuratibu kwa pamoja baina ya pande mbili.
Waziri amesifu kiwango cha kuratibu na kushirikiana kinachokuwa baina ya Wizara hiyo na wizara ya utalii na mambo kale katika kutekeleza matokeo kadhaa ya kimataifa ambayo vyombo vya habari vya kimataifa vimeyasifia kama taratibu za kura ya kombe la mataifa ya Afrika ka mpira wa miguu 2019, pia sherehe za kura ya kombe la Dunia la mpira wa mikono 2021 huko eneo la Piramidi.
Wakati wa mkutano, Dokta Khaled Al Anani alisisitiza hamu ya Wizara ya kuratibu na kushirikiana daima na Wizara ya vijana na michezo, akiashiria kushirikiana kwa Wizara mbili katika kutekeleza matokeo mbali ya kimataifa kama sherehe za kuchukua kura toleo la 27 ya mashindano ya Dunia ya mpira wa mikono kwa wanaume 2021, na mashindano wazi ya Misri ya kimataifa ya Boga “kwa wanaume na wanawake” Misri imeyakaribisha mnamo kipindi Oktoba 10-17 hiyo katika eneo la Piramidi, akibainisha kuwa kukaribisha matokeo makubwa ya michezo katika maeneo ya kihistoria ni njia ya kuonesha Misri ya kiustaarabu na kipekee kwa Dunia, kama kuwa michezo ilikuwa sehemu muhimu katika ustaarabu wa zamani wa kimisri.
Kama Waziri wa utalii na mambo ya kale ameashiria umuhimu wa kupata faida kutoka mashindano ya kimichezo yanayopangiwa nje, haswa yale ambayo mabingwa wa kimichezo wanayacheza, kuyatumia kwa kukuza Misri kimataifa kupitia kuonesha filamu kadhaa za utalii na ukuzaji kwenye maeneo ya utalii ya kimisri, kukuza miradi mikubwa ya kihistoria kama jumba kubwa la makumbusho la Misri litakalofungwa mwaka ujao, pamoja na kusambaza vifaa vya utangazaji wa maeneo ya kihistoria na utalii nchini Misri, kusaidi mashindano makubwa ya kimichezo, hasa Misri inayoyashiriki katika fainali zake, pamoja na kushirikiana baina ya Wizara mbili ili kufanya na kupanga mashindano ya kimichezo haswa nchini Misri.
Waziri wa utalii na mambo ya kale alitangaza kuandaa kwa Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya vijana na michezo katika maonyesho makubwa ya kimataifa ya kiutalii kupitia kushiriki kwa kuonesha miundombinu ya kimichezo, orodha wa matokeo ya michezo, mada zingine, na vifaa vya utangazaji kwa kubaianisha lengo la utalii wa kimichezo nchini Misri, akiashiria kuandaa kwa Wizara kwa kushirikiana Wizara zote katika matokeo hayo ili kubainisha miundombinu ya Misri.
Mwishoni mwa mkutano, mawaziri wawili wamesisitiza umuhimu wa kuenedele kwa kushirikiana baina ya Wizara mbili ili kujenga na kufanya punje kwa bidhaa ya utalii wa kimichezo, haswa inakuwa moja ya mifumo muhimu ya kiutalii inayovutia aina tofauti za watalii, na haswa vijana kutoka mataifa tofauti.
Comments