Waziri mkuu anatumaini juu ya maandalizi ya viwanja vya Ulinzi wa anga na ALSALAM kwa michuano ya kombe la mataifa ya kiafrika kwa Soka

Dokta Mustafa Madbuly "Waziri mkuu", pamoja na Dokta Ashraf Sobhy "Waziri wa vijana na michezo ", Jenerali Khaled Abd Elaal "Gavana wa Kairo", walitembelea viwanja vya ( Alsalam na Eldefaa Elgawy) ALSALAM na Ulinzi wa anga, ili kuangalia maandalizi ya mwisho yanayohusu kuzindua michuano ya kombe la mataifa ya kiafrika kwa Soka itakayofanyika nchini Misri mwezi huu. 

Na mnamo ziara hii waziri mkuu alitafutia shughuli za maendeleo na kuongeza ufanisi uliofanyika katika uwanja wa Ulinzi wa anga unaoweza kujumuika mashabiki elfu 30, na shughuli hizi zilikusanya sakafu ya uwanja na njia ya mbio, mahali pa waandishi wa vyombo vya habari, milango mikuu na midogo, vyoo vya mashabiki, vyumba vya kuvua nguo kwa wachezaji, vyumba vya kiutabibu kwenye uwanja, pia kuongeza idadi ya viti vya chumba, na viti vya wachezaji, ukiongezeka na kuwepo ufikiaji wa mtandao ya intaneti (WI fI) uwanjani.

 

 pia Dokta Mostafa Madbuly alitafutia shughuli za maendeleo zilizofanyika katika uwanja wa Amani, zilizojumuisha pia sakafu ya uwanja, minara, vyumba vya watu muhimu, viwanja vya mashabiki na waandishi wa vyombo vya habari ukiongezeka na vyumba vya kuvua nguo kwa wachezaji, kituo cha kihabari, vyoo vya mashabiki, na marekebisho yanayohusu Kamera na vyumba khasa vya uangalifu kwenye uwanja.

 

  Na mnamo mwisho wa matembezi Waziri mkuu alisifu juhudi zinazotolewa kutokana na taasisi tofauti zinazojali kushiriki katika kuandaa na kupanga michuano, na misaada yao katika kumalizika maandalizi tofauti, na khasa inayohusu majengo ya kimichezo ambapo mechi za michuano hutafanyika, na hayo yote kwa ajili ya kuonyesha Misri kwa picha adhimu inayofaa na kuthibitisha juu ya uwezo wake wa kukaribisha matukio muhimu ya kimichezo.

 

Comments