Katika maandalizi kwa mechi za kiafrika kwa Al-Ahly na Zamalek... Waziri wa michezo akagua uwanja wa Kairo


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikagua vifaa kadhaa kwenye uwanja wa kimataifa wa Kairo pamoja na uwanja mkuu, na kwa kuzingatia maandalizi ya kukaribisha mechi zijazo za Al-Ahly na Zamalek katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya ligi ya mabingwa wa Afrika, utakaofanyika kwenye uwanja mkuu wa uwanja wa kimataifa wa Kairo Ijumaa na Jumamosi zijazo, kwa maandalizi ya mechi ya mwisho ya ubingwa wa Afrika ikiwa mmoja au wote wa Al-Ahly na Zamalek watafikia Fainali ya mashindano.


Kwa upande wake, Dokta Ashraf Sobhy alisema kwamba amefuata mechi za timu tatu za Misri za Al-Ahly, Zamalek na Pyramids kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa na mashindano ya shirikisho, akiashiria kuwa uamuzi wa serikali ya Misri kurudi na kuanza tena mechi za ligi kuu ya mpira wa miguu imelipa kwa utendaji mzuri na matokeo mazuri yaliyopatikana na Al-Ahly na Zamalek wakati wa mechi za kuenda kwenye mashindano ya Afrika.


Pia, Ziara ya Waziri ilijumuisha kukagua ukumbi mkuu uliofanyikwa wa uwanja huo, uliopangwa maandalizi sherehe za ufunguzi na kufunga kwa shughuli za mashindano ya mpira wa mikono ulimwenguni, Misri itakayoandaa mnamo Januari 2021 na mashindano na shughuli zake hufanyika katika kumbi kuu nne, ukumbi uliofanyikwa katika uwanja wa Kairo, Mji mkuu mpya wa kiutawala, 6 Oktober na Borg Al-Arab kwenye pamoja na ukumbi mdogo wa mafunzo.


Waziri wa michezo alihakikishwa wakati wa ziara yake ya ukaguzi na mikutano yake na wale waliohusika na Maendeleo ya ukumbi uliofunikwa mwenyeji wa hafla za kombe la Dunia, kwamba kazi zote zinazoendelea ukumbini zitakamilika na kuwa tayari wakati wa siku zijazo kukaribisha kombe la Dunia.

Comments