Chini ya usimamizi wa Wizara ya vijana na michezo ... Misri yapokea mashindano ya Ocean Man ya kuogelea kwa mara ya kwanza barani Afrika
- 2020-11-01 11:34:02
Mnamo Ijumaa 30/10 , chini ya usimamizi wa wizara ya vijana na michezo mafanikio ya mashindano ya Ocean Man ya kuogelea yalizinduliwa huko Sahl Hashish mkoani Hurdaga kwa ushiriki wa washiriki 600 wanaziwakilisha nchi 11 (Ujerumani - Hungary - Belarusi - Kuwait - Kazakhstan - Falme za Kiarabu - Urusi - Poland - Romania - Ukraine - Italia) pamoja na idadi ya waogeleaji wamisri.
Mashindano ya Ocean Man yanazingatiwa moja ya mashindano ya kuogelea ya muda mrefu baharini kwa umbali wa " kilomita 1.5 kilomita na kilomita 10" pamoja na mashindano ya vikundi.
Inaashiriwa kuwa mashindano ya Ocean Man kwa mara ya kwanza barani Afrika na kwa mara ya pili katika mashariki ya kati baada ya kutoa kwa kampuni ya Boots Egypt faili muhimu ya kupokea mashindano ya Dunia yaliyofanyika katika nchi 20 tofauti kupitia miaka iliyopita .
Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa vijana na michezo alisema kuwa wizara yake inahangaika kufufua utalii wa kimchezo nchini na kuuweka kwenye mpango wa kuitangaza Misri huko nje kupitia mwaliko wa taasisi za Dunia zinazohusika na kupanga mashindano na sherehe kubwa za kimchezo,wakati ambapo Misri ina vivutio vya utalii na uwezo wa kutaratibu shughuli kubwa za kimichezo.
Waziri huyo alieleza kuwa Misri ina aina kadhaa za kimichezo ambazo Dunia yote inazitafutia,na mtazamo wa Wizara katika utalii wa kimichezo ni kusaidia na kuunga mkono mipango ya nchi katika kueneza utalii kwa minasaba na shughuli kubwa za kimichezo,wakati ambapo Utalii wa kimichezo ni njia moja muhimu ya kupanuka vivutio vya utalii haswa akiashiria kuwa una mashabiki wengi duniani kote.
Kwenye muktadha huohuo Fermin Akhido Alonso wa Uhispania , mwanzilishi wa mashindano hayo , akiashiria kuwa kupokea kwa Misri kwa mashindano ha Ocean Man huzingatiwa ongezeko kubwa kwa mashindano , akisifu sana maandalizi ya washiriki na uwezo wa Misri wa kupanga , na hali ya hewa nzuri inayohimiza kupanga mashindano kwa mara nyingi nchini Misri.
Kwa upande wake , Sherif Fathy , mkuu wa kamati iandaayo mashindano , alishukuru Wizara ya vijana na michezo kwa ufadhili wake kwa mashindano ya Ocean Man na kusisitiza Misri kupokea mashindano hayo japo kuwepo kwa changamoto za virusi vya Corona , Pia akashukuru Shirikisho la Misri la kuogelea Yasser Idris na bodi ya uongozi wa Shirikisho Ahmed Abdelkhalek mwakilishi wa Wizara ya vijana na michezo , Sherif Fathy mkuu wa kamati iandaayo mashindano na Farmin Akhido Alonso mwanzilishi wa Ocean Man
Comments