kwenye hafla ya Siku ya Vijana waafrika,kwa mara ya kwanza Waziri wa Vijana apeleka ujumbe kwa vijana wa bara hilo

Sobhy: Muungano wa Afrika huanza kupitia kuunda kizazi wa Kiafrika wanaoliamini.
Sobhy: Misri yatoa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi kuwezesha kuhamisha uzoefu wa maendeleo wa Misri katika ujenzi wa taasisi na mhusika wa kitaifa.
Profesa Ashraf Sobhy, Waziri huyo, alitoa hotuba kwa vijana waafrika kwa lugha kadhaa, nazo ni Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili, ndani na nje ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, ambapo alipoelezea furaha yake kubwa kwa diplomasia ya vijana inayofanya kazi barani Afrika, akiwapongeza kwa hafla ya "Siku ya Vijana waafrika", ambapo vijana waafrika wanaposherehekea mnamo Novemba Mosi ya kila mwaka tangu Hati ya Vijana ya Afrika ilipopitishwa mnamo 2006.
Waziri huyo, wakati wa hotuba yake alisisitiza kwamba uongozi wa kisiasa nchini Misri ukiongozwa na Rais Abd El-Fatah El-Sisi una nia ya kusaidia na kuwawezesha vijana waafrika kupitia misaada ya kuwezesha inayotolewa na Misri pamoja na misaada maalum ya kiufundi inayotolewa na mamlaka na Wizara za Misri, inayochangia kufungua upeo wa maendeleo na kuhamisha uzoefu na tamaduni katika nyanja kadhaa.
Ashraf Sobhy alitoa taarifa ya maelezo kwa vijana wa bara la Afrika, ili kudhibitisha azma ya uongozi kwenda kusini na kushikilia maadili ya Muungano wa Afrika na watu wa bara hilo, sio tu kwa maneno matupu bali kwa vitendo halisi na pia kudumisha thamani ya ushirikiano (Kusini Kusini), akionesha kuwa nchi ya Misri, ikiwakilishwa na Wizara ya Vijana na Michezo, kwa kushirikiana na Wizara na taasisi nyingi , mnamo kipindi cha miaka kadhaa imekamilisha shughuli nyingi za vijana barani kuunga mkono mpango wa Umoja wa Afrika "kuwawezesha vijana wa kiume na kike milioni ifikapo 2021, inayojulikana kama 1Mby2021, wakati wa Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika mnamo 2019, ambayo ya kwanza ni Tangazo la Rais wakati wa Mkutano wa Vijana Duniani, "Aswan ni mji mkuu wa vijana waafrika."
Misri ilipokea mashindano na sherehe nyingi wakati wa 2019 /2020, haswa (Mashindano ya Soka ya Mataifa ya Afrika kwa Wakubwa, ambayo Misri iliandaa baada ya kutokuwepo kwa takriban miaka 13 na ushiriki wa timu 24 kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano na ufunguzi wa hadithi unaofaa historia ya Afrika / Mashindano ya Mataifa ya Afrika chini ya miaka 23 kufikia Olimpiki ya Tokyo 2020 na ushiriki wa timu 8 za Kiafrika zilizofikia Mashindano ya Afrika / Mashindano ya Kuinua vyuma kwa Vipofu), na Wizara ya Vijana na Michezo iliandaa programu nyingi wakati wa 2020, haswa (Michezo ya Kwanza ya Afrika ya Olimpiki Maalum chini ya Usimamizi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi / Baraza la Vijana la Kiarabu na Afrika huko Aswan chini ya Usimamizi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, pamoja na ushiriki wa vijana waafrika na waarabu zaidi ya 1500 / Jukwaa la Vijana la Kiafrika juu ya Uraia na Maendeleo kwa ushiriki wa nchi 20 za Kiafrika / Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Afrika chini ya Uongozi wa Waziri Mkuu Dokta.Mustafa Madbouly na kwa ushiriki wa vijana wa kiume na kike 120 kutoka nchi 43 za Afrika / Mpango wa Wajitolea wa Umoja wa Afrika, kundi la kumi, chini ya uongozi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, pamoja na ushiriki wa vijana wa kiume na kike 200 kutoka nchi 54 za Kiafrika, ndio maana ni mpango mkubwa zaidi wa kujitolea barani / Shindano la Ubunifu wa Afrika/ Kuandaa Sherehe ya CAF ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa mwaka 2019 huko Hurghada / Uzinduzi wa safari ya kwanza ya Utalii na utamaduni wa Mto Nile kwa vijana wa Afrika iliyoanza kutoka Kairo hadi miji ya Luxor na Aswan kutoa dhana ya ushirikiano kati ya watu wa nchi za Bonde la Nile / Kupokea Kombe la Dunia la Kupiga Mbizi / Misri ni nchi ya kwanza katika historia ya Afrika kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Ulimwenguni ya Kupiga Mbizi / Kupokea Mashindano ya kombe la Dunia la Boga,na Misri itaendelea kuandaa mashindano hayo hadi 2022.
Kwa kiwango cha hafla za bara na kimataifa, Sobhy aliwapongeza vijana wa Misri ,wawakilishi wa Afrika katika vikao vya kimataifa vya michezo kwa kushinda Kombe la Dunia la Mpira wa Mikono kwa mara ya kwanza katika historia kama timu ya kwanza ya Afrika kutwaa michuano / timu ya Bowling(kupiga mipira) ya Misri ilishinda nafasi ya kwanza kwenye Mashindano ya Mataifa ya Afrika / vijana wa Misri wakivunja rekodi kwenye Michezo ya Afrika kwa medali 273, ikilinganishwa na 217 mnamo 2015 / timu ya Misri ikiwakilisha Afrika kwa mpira wa wavu chini ya miaka 19, ikishika nafasi ya nne Ulimwenguni 2019.
Sobhy alionesha kuwa serikali ya Misri, katika sekta na taasisi zake zote, inafanya juu chini kuwahudumia vijana waafrika na kufikia ushirikiano wa Kiafrika katika Taaluma na nyanja tofauti.
Akihitimisha hotuba yake, Sobhy alieleza utayari wa Wizara ya Vijana na Michezo kushirikiana na kuratibu na mashirika na taasisi za Kiafrika, pia alisisitiza mchango wa Ofisi ya Vijana wa Afrika kama kitengo maalumu kwenye Wizara hiyo kwa masuala ya Afrika na inatarajiwa kufanyika kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi baada ya mafanikio makubwa ya kundi la kwanza.
Ikumbukwe kuwa bara la Afrika lasherehekea, mnamo Novemba Mosi ya kila mwaka, tangu 2006, "Siku ya Vijana wa Afrika."
Tangu Hati ya Vijana ya Afrika ilipopitishwa katika Kilele cha Banjul mnamo 2006, umuhimu wa Siku ya Vijana wa Afrika umekuja kumkumbusha daima mtoaji uamuzi wa haki na mchango wa vijana katika mabadiliko ya kijamii, ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu katika pembe zote za jamii ya Afrika, pamoja na kuelekeza nguvu bora ya vijana kukuza juhudi kuelekea kuhakikisha maendeleo endelevu barani Afrika.

Comments