Waziri wa vijana na michezo apokea mwenzake wa Lebanon


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo aliwapokea Mkuu wa ofisi ya kiutendaji ya mawaziri wa kiarabu wa vijana na michezo, Bibi Fartine Ohanian ambaye ni Waziri wa vijana na michezo wa Lebanon, kutafutia njia za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za vijana na michezo.


Wakati wa ziara, Waziri wa vijana na michezo wa Lebanon alisisitiza kina cha mahusiano thabiti kati ya watu wa Misri na Lebanon, na akaonesha kwamba anatarajia ushirikiano zaidi kati ya nchi hizo mbili katika nyanja tofauti zinazohusiana na vijana na michezo.


Ohanian alisifu juhudi za Dokta .Ashraf Sobhy wakati wa muda uliyopita,aliongeza kwamba Misri ilikuwa na miundombinu ya michezo na vijana kwa kiwango cha juu na inaweza kuwa mwenyeji wa hafla kubwa za kimataifa za michezo na hafla wakati wowote, iliyoonekana wakati wa mwisho baada ya kuanzishwa kwa mashindano makubwa zaidi ya kimataifa, na mabara huko Misri, na pia hafla nyingi za vijana.

Kwa upande wake, Waziri wa Vijana na Michezo alithibitisha shukrani yake kwa Waziri wa Vijana na Michezo wa Lebanon, akiashiria kuwa kipindi kijacho kitashuhudia itifaki nyingi za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja za vijana na michezo. 


Mwishoni wa mkutano, Waziri wa vijana na michezo alimkabidhi mwenzake wa Lebanon bendera na hati iliyoandaa Mkutano wa thalathini wa Skauti wa Kiarabu 2022,  uliohudhuriwa na Misri katika kikao chake cha awali huko 2019, kwa mila ambayo ni ya kwanza ya aina yake katika kiwango cha shughuli za Mkutano wa Skauti ya Kiarabu.

Comments