Waziri wa vijana na michezo awahimiza wajitolea wanaochaguliwa kwa programu ya mazoezi ya michuano ya dunia kwa mpira wa mikono


Dokta Ashaf Sobhy - Waziri wa vijana na michezo - alikutana na wajitolea 500 waliochaguliwa kushirikiana katika programu ya mazoezi  ya toleo la 27 la michuano ya dunia kwa mpira wa mikono wa wachezaji wanaume - Misri 2021 na hivyo kwenye Jukwaa la Wizara ya vijana na michezo.


 Waziri huyo pamoja na wajitolea alisema " kuna ujali mkubwa kutoka viongozi wa kisiasa kwa ajili ya kufanikisha michuano na kuidhihirisha    kwa sura inayofaa nafasi ya Misri ,  na taasisi zote za nchi  zinashirikiana ili kuifanikisha michuano ya dunia ya mpira wa mikono , Misri 2021 ".


Dokta Ashaf Sobhy aliongeza kusema :"Rais  Mheshimiwa Abd El-Fatah El-Sisi anasisitiza mara kwa mara jukumu la vijana katika nyanja zote , na vijana ndio  ni thamani za maana ambazo inawezekana kuziwekeza  na nguvu zake "


Waziri huyo alisisitiza kwamba Misri ina uwezo mkubwa unaoiwezesha kufanikisha jambo lolote linalofanyika ndani ya Ardhi yake  na miongoni mwao uwezekano na  uwezo huo ni thamani za vijana . 

 

 Sobhy alifafanua kuwa kuna uchunguzi unaoendelea kwa michuano na maandalizi yake unatolewa na  Dokta Mustfa Madbouly - Waziri Mkuu na Mkuu wa kamati ya juu ya michuano - , vilevile , kuwepo ziara za nyanjani  mara kwa mara kwa kumbi ambazo michuano itafanyika ndani yake na hivyo kwa ajili kufuatilia maandalizi ya kumbi hizo .


Waziri huyo alisifu  kamati ya wajitolea ya michuano , akieleza kwamba wajitolea wana  kazi muhimu na jukumu kubwa ili kuonesha michuano kwa sura inayohitajika , akifafanua kuwa mtazamo wa kwanza wa wajumbe wanoshirikisha katika michuano unakuja kupitia mawasiliano ya kwanza baina ya wajumbe hawa na wajitolea ".

Comments