Waziri wa vijana na michezo afungua mkutano wa " Uvukaji wa Oktoba " kwenye kituo cha elimu ya kiraia huko Al Jazera
- 2020-11-06 19:55:55
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo , Alhamisi asubuhi , alizindua mkutano wa " Uvukaji wa Oktoba kuanzia 73 hadi 2030 " , ulioandaliwa na kituo cha Nile cha vyombo vya habari huko Kairo kihusianacho na Taasisi kuu ya huduma ya taarifa, pamoja na Muungano wa wanafunzi wa Tahya Masr.
Shughuli za mkutano zinateklezewa huko kituo cha elimu ya kiraia huko Al-Jazera na unajumuisha vikao vitatu vya majadiliano vilivyotolewa na Hisham Abu El maati mkuu wa kituo cha Nile cha Vyombo vya habari huko Kairo ambapo kikao cha kwanza kitajadili " mkutano wa vizazi .. roho ya Oktoba " na wasemaji wake ni Jenerali Naser Salem, Mkuu wa zamani wa shirika la upelelezi na mtalaam wa mambo ya mkakati na Mhandisi Mustfa Salem , kikao cha pili kinakuja chini ya kaulimbiu " miradi ya kitaifa kulingana na mkakati wa Misri kwa maendeleo ya endelevu 2030 " hivyo hutolewa na Dokta Youssef Werdany , Msaidizi wa Waziri wa vijana na michezo , Dokta Hussen Abaza , Mkurugenzi wa kitengo cha mtazamo wa Misri 2030 kwenye wizara ya Upangaji .
Wakati ambapo kikao cha tatu ni mazungumzo ya kuwawezesha vijana Ujasiriamali" miradi midogomidogo na wastani " kwa kushirikiana na Dokta Ahmed El Masry wakili wa taasisi ya kitaifa ya miradi midogomidogo na wastani na Dokta Ahmed El-shrif katibu mkuu wa taasisi ya viongozi wa mambo ya usimamizi , vilevile , mkutano unajumuisha maonesho ya kisanaa kadhaa .
Na wakati wa matamshi ya ufunguzi ya mkutano , Dokta Ashraf Sobhy aliashiria kwa utiliaji mkazo wa Rais Mheshimiwa Abd El-Fatah El-sisi Rais wa Jamhuri kwa vijana wa Misri na kutilia mkazo kuendeleza ufundi wao na kuwawezesha katika nyanja mbalimbali , akiashiria inapaswa tukubaliane kuendesha uwezo wetu katika huduma ya nchi yetu , na kufanya kazi ili kujiendeleza nafsi kwa elimu na masomo na kukabiliana changamoto .
Waziri wa vijana na michezo alieleza kwamba Uvukaji wa Oktoba unazingatiwa kiashirio ya mafanikio , kupanga , subira na kuleta uwezo kwa kuwa mojawapo ya sifa wazi zaidi ya jeshi ya Misri , akiashiria kuwa mabadiliko ya maendeleo ambayo nchi inayapata sasa hivi ni hayawahi kuwepo na yazingatiwe kuvuka kwa mustakabali inayotarajiwa.
Waziri alitaja katika kauli yake juhudi za nchi zinazofanyiwa ili kupambana na ugaidi kupitia mikono ya jeshi na polisi wa Misri ili kulinda Misri na raia wake , akibainisha kuwa vijana wa Misri wakawa na ufahamu wa kweli kwa changamoto mengi yanayokubali nchi .
Kwa upande wake , Dokta Taya Abd El latef , Mshauri wa Waziri wa elimu ya juu kwa shughuli za wanafunzi : " Misri yahitaji vijana wake , na kuna changamoto kadhaa , maadui, na majasusi kadhaa kwa nchi , jambo linalotuhitaji sisi sote tushikamane ili kukabiliana na mambo hayo " , akibainisha kuwa alitambua wakati wa mikutano yake na vijana wanaoshirikisha katika mkutano kabla ya kufanyika kwake kwamba matakwa yao yanasambamba na mtazamo na pango wa mkakati wa Wizara ya vijana na michezo .
Wakati ambapo Dokta Nadia Mahamoud, Mratibu Mkuu wa kituo cha Nile cha Vyombo vya habari alipofafanua kuwa kuimarisha maelewano ya aina za jamii kwa masuala mbalimbali ni jukumu muhimu zaidi la majukumu ya taasisi kuu ya taarifa , na aina muhimu zaidi ya aina hizo ni vijana na kupanga kila kitu pamoja nao kwa kiwango cha Jamhuri ili kutekeleza programu za kutoa nasaha .
Comments