Wapenzi wa mpira wa miguu wanasubiri miadi mpya kati ya nguzo mbili za mpira wa miguu za Misri-Al Ahly na Zamalek kwa mara ya kwanza katika historia ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.
Timu nyekundu ilifikia fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kushinda Wydad ya Morocco kwa mabao matano kwa bao moja tu, kwa jumla ya michezo miwili.
Wakati Timu nyeupe ilifikia fainali baada ya kushinda Raja ya Morocco, kwa mabao manne kwa bao moja tu,kwa jumla ya michezo miwili.
Hii ni mara ya kwanza kwamba nguzo mbili za mpira wa miguu wa Misri kukutana na fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika, na pia ni mara ya kwanza kwamba pande mbili za fainali ya Afrika zinatoka kutoka nchi moja.
Timu hizo mbili imepangwa kukutana 27 mwezi huu saa tatu jioni.
Timu hizo mbili zilikuwa zimekutana hapo awali kwenye mashindano haya katika mechi zaidi ya moja, lakini muhimu zaidi ilikuwa katika nusu fainali mnamo 2005, ambapo Al-Ahly ilishinda mpinzani wake wa jadi kwenda na kurudi , na kufikia fainali kushika lakabu.
Ikumbukwe kuwa Klabu ya Al-Ahly imepata idadi kubwa zaidi kwenye mashindano haya, ambapo imeyashinda mara 8, na Klabu ya Zamalek inashika nafasi ya pili, ikiyashinda mara 5.
Comments