Waziri wa Michezo asifu uteuzi wa mwenyekiti wa Shirikisho la kujenga mwili kama msimamizi bora duniani kutoka Shirikisho la Kimataifa

 Akisisitiza uungaji mkono wa Wizara kwa Makada wa kimchezo wa kimisri


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisifu uteuzi wa Shirikisho la Kimataifa la Ujenzi wa mwili kwa Dokta Adel Fahim kama mwenyekiti wa Shirikisho la Misri la Ujenzi wa mwili,Mwenyekiti wa Shirikisho ya Kiarabu na Afrika, na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Kimataifa kama msimamizi bora kwa kiwango cha mchezo huo duniani , akimpongeza kwa kupata ngao ya roho ya ujasiri yenye nafasi ya juu kabisa kutoka  Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Ujenzi wa mwili.


Waziri huyo alisisitiza uungaji mkono wa Wizara hiyo kwa makada wa kimichezo wa kimisri, na kuwahimiza kufikia mafanikio , yanayoonekana kwenye maendeleo ya mfumo wa michezo, akisifu jukumu la Mwenyekiti wa Shirikisho la Kuijenga mwili katika kueneza mchezo huo katika ngazi zote, iliyochangia kuheshimiwa kwake na Shirikisho la Kimataifa baada ya mkutano wa Jumuiya kuu kwa  Shirikisho la Kimataifa  huko Uhispania pembezoni mwa Mashindano ya Dunia ya Ujenzi wa mwili.


Waziri huyo alidokeza ufuatiliaji kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na  Kamati ya Olimpiki ya Misri na mashirikisho yote ya michezo katika kutekeleza utaratibu wa kupanua uenezaji wa michezo yote katika mikoa yote, pamoja na kuangalia vifaa na maandalizi ya wachezaji wa timu ya kitaifa kwa mashindano tofauti .  Ili ulimwengu ushuhudie maendeleo ya michezo ya kimisri,sawa iwe katika kiwango cha ushindani au kiwango cha akili katika kusimamia mfumo wa michezo,na hivyo katika muktadha wa kutembea kando ya njia ya mafanikio yaliyoshuhudiwa na mchezo wa Misri hivi karibuni.

Comments