Waziri wa Michezo ahudhuria toleo la tatu la tamasha la parashuti , "Ruka kama Farao" juu ya piramidi
- 2020-11-11 11:15:36
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo,mnamo mchana wa leo amehudhuria shughuli za tamasha la kuruka kwa parashuti juu ya paa la piramidi, linalofanyika chini ya kauli mbiu "Ruka Kama Farao" katika toleo lake la tatu na lililoandaliwa na utawala mkuu wa utalii wa kimchezo kwenye Wizara ya Vijana na Michezo chini ya usimamizi wa Shirikisho la kimisri la parashuti na Michezo ya Anga.
Washiriki 120, walishiriki katika tamasha la Ruka kama Farao"Jump like a Pharaoh Vol 3" katika toleo lake la tatu, wakiwakilisha Misri, Marekani, Brazil, Ufaransa, Uingereza, Ubelgiji, Uholanzi, Uswizi, Kroatia, Urusi, Italia, Ujerumani, Emirates, Kuwait, Morocco, Canada, Saudi Arabia, Uchina, na kuruka kutoka kwa ndege ya C 130 na kutoka urefu wa futi 15,000, juu ya piramidi za Giza.
Wakati wa sherehe hiyo, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alithibitisha kwamba tamasha la ruka kama farao ni moja ya hafla muhimu zaidi ya michezo ya watalii ambayo Wizara ya Vijana na Michezo inataka kuifanya kwa sababu ya umuhimu wake mkubwa wa michezo na utalii, na hivyo ilivyofanyika kupitia Wachezaji 120 kutoka nchi tofauti za ulimwengu, akiongeza kuwa wale wanafanya kazi kama mabalozi kwa Misri ili kupeleka picha ya michezo na utalii ya Misri kwa nchi zao katika ujumbe wa Amani kutoka Misri, nchi ya ustaarabu kwa sehemu zote za ulimwengu, akiwaalika watu ulimwenguni kutembelea Misri kwa hali ya Usalama na Amani inayopatikana nchini Misri.
Waziri huyo aliongeza kuwa Ajenda ya Wizara ya Vijana na Michezo ni pamoja na kufanya hafla nyingi kuu za michezo katika maeneo kadhaa tofauti ya utalii na akiolojia ya Misri.
Ikumbukwe kuwa toleo la tatu la tamasha hilo lilipangwa kuzinduliwa Juni iliyopita, lakini mazingira ya mlipuko wa Janga la Corona ulimwenguni yalizuia kushikiliwa kwa sababu ya kusimamishwa kwa harakati za ndege.
Tamasha hilo lilihudhuriwa na Ahmed Abdel Khaleq, Mkurugenzi Mkuu wa Utalii wa Michezo kwenye Wizara ya Vijana na Michezo, na washiriki kadhaa wa Shirikisho la Misri la parashuti na michezo ya Anga.
Comments