Hotuba ya Rais El-Sisi mwishoni mwa Mkutano Wa Vijana Wa Kiarabu na Afrika Mjini Aswan
- 2019-04-01 16:11:48
“Kwa jina la
mwenyezi mungu mwingi wa rehema, mwenye kurehemu “
Binti zangu,
watoto wangu.Vijana wa Waarabu na Waafrika ,ndoto yetu katika siku zijazo.
Mabibi na Mabwana
,Waheshimiwa mliohudhuria.
Mwanzoni
ninawapongezeni wote mliohudhuria ,
Waandaaji , Vyombo na taasisi za
Serikali juu ya mafanikio ya Matokeo ya Mkutano huu na kufaulu hali hii nzuri
yenye matumaini ambayo yameambatana nasi kwa siku mbili mfufulizo,
nakuhakikishieni wote kwamba hisia
na ufahari uliochanganyika na furaha, wakati nikifuatilia kwa kina wasomi hawa hodari
miongoni mwa vijana wetu wa Kiaraabu na Kiafrika, na niwashukuru sana vijana wa
Misri walioweza kuandaa jukwa hili la majidiliano na ubunifu ambao umetupa fursa kwa wote kubadilishana mawazo na
mtazamo,vijana wetu wa Kiarabu na Kiafrika Wametengeneza mfumo bora wa kuigwa
na unawezekana kutegemewa katika kujenga mazungumzo ya kina, pia wamesisitiza kwamba ukamilifu
wetu wa Kiarabu na Kiafrika ni lengo linaloweza kufanikiwa.
Hakuna shaka
kwamba tofauti zetu ni thamani ambayo inaongeza kuimarisha mshikamano na
haijawahi kamwe kuwa sababu ya migogoro na mapambano.
Nilikuwa na
furahi kubwa sana kwa mifano ya vijana hawa, vijana wanaohimiza ubunifu na
wanaolenga kuhakikisha siku zijazo na kuitengeneza mustakbali, ulio jaa Amani na utulivu kwa wanadamu wote,
na siku baada ya siku inathibiti katika moyo wangu kwamba upendeleo wangu kwa
vijana wa Misri na ndoto zao,ujasiri,shauku usafi wao ulikuwa ni upendeleo
Sahihi, na dalili ya kina ya kwamba matokeo yaliyotolewa maono na mapendekezo ni yenye uwezo wa kutumika na kutekelezwa.
Hakika Hali halisi ambayo tunakabiliana nayo
leo, ambayo imeambatana na machovu ya vita, migogoro na kupotoka mno kwa mfumo wa kibinadamu ambapo haijapata kutokea,
inatulazimisha kuimarisha juhudi zetu ili kurejesha na kuboresha majadiliano ya
kibinadamu na kuunda mustakbali wa ubinadamu, ambao unajumuisha maana ya utulivu,
amani na maendeleo na kuondokana na migogoro ambayo ambayo inakaribia kuharibu
ulimwengu wa leo. Na hatuna budi ila
kushikilia wajibu wetu wa kihistoria na wa kibinadamu na tunapaswa kusimama
nyuma ya matarajio yote ya vijana wa
dunia na kuwekeza nguvu na mawazo yao katika mradi wa kujenga mustakbali, na
kuimarisha maadili ya kiustaarabu, kiubinadamu, amani na haki.
Vijana wa
Misri, Kiarabu na kiafrika Ninawausieni
kushikamana na ndoto zenu na kujitahidi
ili kuzifanikisha, bila ya kupotoka kutoka kwenye malengo yanu ya juu ..
Jitahidini sana kwa ajili ya mustakbali
wenu na mustakbali wa nchi zenu, fanyeni mahujiano na majadiliano na kukubali
wengine iwe ni katiba yenu ,na ubinadamu ni sheria yenu na kazi ni njia yenu ..
fanyeni bidii ili kuhakikisha amani na utulivu nchini mwenu .. fanyeni kazi Na vita vyenu kwa ajili malengo mazuri
ni vita vyenu vya juu zaidi, hifadhini
usafi wenu wa nyoyo na shauku na msitoke kwenye mfumo wa kibinadamu wa kimsingi.
Nashukuru jitihada zenu halisi zilizofanikiwa wakati wa matukio haya ya Mkutano wenye
mafanikio, kwa hakika mimi ninapendekeza
mapendekezo ninayoyaamini.
kwa hivyo niliamua:
Kwanza: Baraza la Mawaziri kwa kushirikiana na
Wizara ya Mambo ya Nje na Elimu kufungua mlango kwa ajili ya kushiriki ya
watafiti kutoka nchi za Kiarabu na kiafrika ili
kufaidika na Benki ya Maarifa ya
Misri na kupitia njia sahihi ili kulitekeleza hilo.
Pili, Wizara
ya Elimu ya Juu kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha kutoa mafunzo na kuwaandaa vijana kuanzisha Baraza la
Ushirikiano kati ya Vyuo Vikuu vya Kiarabu na vya Afrika ili iwe njia jukwaa
bora ya kuimarisha ushirikiano wa kisayansi na kitamaduni kati ya Waarabu na
Afrika.
Tatu, Wizara
ya Afya kwa ushirikiano na vyombo na taasisi zote zinazohusika nchini
kutekeleza mpango wa Misri kwa ajili ya
kumambana na virusi «C» kwa waafrika milioni na kuanza awamu mpya ya
kampeni ya afya kwa milioni100 » ili
kukomesha virusi «C» kwa wakazi wageni waishio nchini Misri na siwaiti wakimbizi.
Nne: Idara
ya Mkutano wa Vijana wa dunia iunde timu ya vijana wa Kiarabu na Kiafrika ili
kuandaa mtazamo maalumu wa kufikia fursa za ushirikiano wa Kiarabu na Afrika
katika nyanja zote na kuwasilisha mamlaka husika katika nchi zetu ili kuanza
utekelezaji.
tano: Idara
ya mkutano wa Vijana wa dunia kuunda
timu ya kazi ya vijana wa kiarabu na kiafrika ili kuweka maono ya vijana kwa
njia ya kushughulikia maswala ya uvuto wa kifikri na msimamo mkali na
kuyawasilisha kama mpango wa vijana ili kumaliza ugaidi na msimamo kikali.
Sita: Idara
ya Jumuiya ya Vijana wa dunia kuandaa
mkutano wa Misri na Sudan ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi mbili
chini ya msingi wa udugu wa bonde la Nile.
Saba: Kwa
mujibu ya jukumu la Umoja wa Afrika, Misri huandaa karatasi kwa kushirikiana na
Tume la Umoja wa Afrika katika uratibu na Tume ya Umoja wa Afrika na taasisi ya nchi za Kiarabu ili
kuwasilishwa kwenye Mkutano wa pili wa Kiarabu na wa Afrika ambao unajumuisha
mapendekezo maalumu na ya kikazi katika nyanja tatu zifuatazo:
Uanzishwaji
wa soko la pamoja la Kiarabu na Afrika.
Kuanzishwa
mfuko wa kufadhili miundombinu ya Mawasiliano ya Afrika katika maeneo ya
barabara, reli na umeme ili kukuza ushirikiano wa bara.
Kuanzishwa
mfumo wa Kiarabu na Afrika wa kupambana na ugaidi na kufikia usalama na
utulivu.
Nane: Kujishughulisha
na kutumia Vyombo vya habari na Mitandao ya Kijamii ili
kuondoa dhana potofu kuhusu mahusiano ya
kiafrika na kiarabu .
Tisa:
Kufanya hima ili kuwawezesha
vijana na wanawake ili kubadilisha Utashi wa kisiasa kwenye hatua ya vitendo kwa
ajili kuwaandaa kupitia kuboresha elimu
na mafunzo.
Mabibi na Mabwana
Binti zangu
na wanangu,Waheshimiwa mliohudhuria
wazo ni
mwanzo wa ndoto na kwa
kiwango cha imani kwenye ndoto hupatikana,
na binadamu
wanahitaji ndoto za vijana na matumaini kwa safari ya baadaye, msingi wake ni
usafi katika nia na jitihada kwenye kazi
na imani kamili kwamba amani na haki ni njia pekee ya binadamu halisi na
ulimwengu wenye utulivu na kufikia ubora wa maisha ya mwanadamu.
Mwishoni,
sina la kusema kwenu isipokuwa kuwakaribisheni daima katika nchi yane ya pili,
Misri
Ninawaambia
vijana wote walio pamoja nasi kwa sasa na kila mtu ambaye ananisikia mimi,
tafadhali hifadhini nchi zenu .. Misri Ibakiwe, na Mataifa yetu ya Kiarabu na Bara letu la
Afrika.
Rehma na Amani
ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu.
Comments