Waziri wa michezo ashuhudia mkutano wa waandishi wa habari kwa mashindano ya urafiki ya timu za Olimpiki
- 2020-11-11 11:25:32
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa vijana na michezo alishuhudia mkutano wa waandishi wa habari kwa mashindano ya urafiki ya timu za Olimpiki chini ya miaka 23 , kilichopangwa na Misri kwa ushiriki wa timu za Brazil na Korea ya kusini pamoja na timu ya kitaifa ya kiolimpiki mnamo kipindi cha ( 12_17) Novemba hii , kwenye mfumo wa kuandaa kwa ushiriki katika Olimpiki ijayo ya Tokyo .
Mkutano huo ulihudhuriwa na Amr Elganayni, Mwenyekiti wa kamati ya pande tano iliyotumiwa na uongozi wa shirikisho la kimisri la mpira wa miguu , na Kocha Shawky Gharib Mkurugenzi wa timu ya kolimpoki , na Kocha wa timu ya kiolimpiki Naser Maher , Sekretarieti wa kwanza wa Mkuu wa Shirikisho la Brazil na mwenyekiti wa ujumbe _ Wrikardo Lema , mchezaji Rogrejo wa Rial Madrid na timu ya Brazil , Kem Hagom mkurugenzi mtendaji wa timu ya Korea na mchezaji Kim Diwan wa timu ya Korea .
Wakati wa hotuba yake , Waziri wa vijana na michezo alisisitiza kuwa nchi ya Misri inatoa ufadhili wote kwa ubingwa na kwa timu ya kiolompiki na timu za kitaifa kwa aina zake zote kwenye mashindano yajayo . akibainisha kuwa ubingwa huo unazigatiwa kama tukio muhimu kwa timu ya kiolimpiki wakati wa ushiriki wa timu ya Brazil yenye toleo la mwisho la Olimpiki Riody Janiro 2016 , akiongeza kwamba timu ya kiolimpiki ya kimisri itapewa ufadhili wote kutoka kwa uongozi wa kisiasa unaofadhili sekta ya kimchezo daima .
Sobhy akasifu juhudi zinazofanywa na Shirikisho la kimisri la Soka kupitia kipidini kilichopita na ufadhili wake mzima kwa timu za kitaifa ili kufanikisha mafanikio ya kimchezo kama ilivvyotokea na timu ya kiolimpiki na ushindi wake wa ubingwa wa Afrika chini ya miaka 23 , uliofanyika mwaka jana na kufikisha timu ya kiolimpiki kwa Olimpiki ya Tokyo .
kwa upande wake , Omar Elganayny amemshukuru Waziri huyo kwa msaada wake wa kudumu kwa mchezo na wachezaji kwenye michezo yote , pia akashukuru timu zinazoshirki katika mashindano ya urafiki kwa kukubali mwito , akitamani ubingwa uwe mzuri sana na timu ya kiolimpiki ya kimisi ipate faida kubwa kutokana na mechi hiyo yenye nguvu na timu amabzo ni bora zaidi kwa Kiwango cha timu za kiolimpiki .
kwa upande wake , mwenyekiti wa ujumbe wa timu ya kiolimpiki ya Brazil alisifu uzuri wa kupokea , pia alisifu Kiwango cha kiutendaji cha timu ya kiolimpiki ya kimisri , akitarajia usalama na afaya kwa wachezaji wote wanaoshiriki kwenye ubingwa .
Mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya Korea alishukuru serikali ya kimisri kwa ufadhili wake kwa ubingwa huo , akashukuru Shirikisho la kimisri kwa kupanga ubingwa kwenye muda huo mgumu ambao nchi zote za ulimwenguni zinaupatia .
Mechi ya kwanza inafanyika tarehe 12 Novemba mbele ya timu ya Korea kusini , wakati mechi ya pili itafanyikwa mbele ya timu ya Brazil tarehe 14 ya mwezi ule ule .
Timu ya Misri ya kiolimpiki ilikuwa imepewa taji la ubingwa wa kombe la mataifa ya kiafrika yaliyokaribishwa na Misri mwaka 2019 kwa uongozi wa Shawky Gharib ili kufikia Olimpiki ya Tokyo iliyoaharishwa ifanyike mwaka 2021, kwa ajili ya virusi vya Corona.
Comments