Waziri wa michezo na Mkuu wa Baraza la juu la vyombo vya habari wazindua mpango wa " Misri ipo kwanza na Hapana kwa Kutovumiliana"


Waziri wa vijana na michezo Dokta Ashraf sobhy na mwandishi wa habari Karam Gaber, Mkuu wa Baraza la juu la vyombo vya habari walizindua siku ya Alhamisi Mpango wa "Misri ipo kwanza na Hapana kwa Kutovumiliana" kwa mahudhurio ya Wataalam kadhaa wa vyombo vya habari.


Mpango huo ulikuja katika mfumo wa kujiandaa kwa mechi ya fainali ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa  Afrika iliyopangwa kufanyika kati ya timu ya Al-Ahly na Zamalek ,  Novemba 27, na unaalika vyombo vya habari ili kujitolea kwa kanuni za utangazaji wa vyombo vya habari kwa mechi ya fainali ya mashindano ya Afrika na kutekeleza udhibiti unaohifadhi ujumbe wa michezo na kuhamasisha roho ya michezo baina ya mashabiki wa klabu mbili.


Na katika hotuba yake , Dokta ashraf sobhy alisifu ushirikiano wenye mafanikio pamoja na Baraza la juu la vyombo vya habari katika uzinduzi wa mpango wa " Misri ipo kwanza na Hapana kwa Kutovumiliana" Ili kusambaza maadili na roho ya michezo kati ya mashabiki wamisri mnamo wakati muhimu huu .


Na Waziri huyo alionesha kwamba mpira wa miguu unategemea wachezaji , Mashabiki , klabu , Shirikisho la mpira

Na vyombo mbalimbali vya habari  katika Taasisi kamili ya michezo , akiashiria kwamba vyombo vya habari ni Mshiriki wa mafanikio ya juu na nguvu chanya zinaambatana na nchi ya Misri 



Waziri huyo akiashiria kwamba mpango wa " Misri ipo kwanza na Hapana kwa Kutovumiliana" Haitoshi tu kwa mechi ijayo ya Al Ahly na Zamalek katika fainali ya Afrika , lakini sisi tunaelekea kutekeleza Kampeni zinazoendelea  ili kujadili umuhimu wa kukataa kutovumiliana katika nyanja ya michezo na kufikia kuweka Udhibiti maalum kwa Taasisi. 


Na kutoka upande wake mwandishi wa habari Karam Gaber alibainisha kwamba vyombo vya habari vina jukumu muhimu katika kukabili kutovumilana kwa michezo na kutotumia njia yoyote inayoudhi mashabiki na kuwachokoza , akiashiria kwamba mikutano kadhaa ya mazungumzo itafanyika na kuweka mpango wa kila mwaka na warsha kwa uratibu wa Wizara ya vijana na michezo ili kujadili njia za kukabili kutovumilia na kuhifadhi maadili ya kimchezo.


Idadi kadhaa wa wataalam wa vyombo vya habari , Wahariri wengi wakuu , mwandishi mkubwa wa habari

Salah Montaser  , Dokta Kamal Darwesh na idadi kadhaa ya Watoa programu za talk show na programu za kimchezo, wote walihudhuria mkutano huo.

Comments