Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alikuwa na hamu ya kuhudhuria mechi ya timu ya kitaifa ya Misri na Togo katika raundi ya tatu ya kufikia Kombe la Mataifa ya 2022 huko Cameroon kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kairo.
Waziri wa Vijana na Michezo, alikuwa pamoja na Amr Al-Ganaini Mwenyekiti wa Kamati ya Miaka Mitano anayesimamia Shirikisho la Soka la Misri, Dokta Gamal Mohamed Ali Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo na wajumbe wa Kamati hiyo Dokta Ahmed Abdullah, Dokta Sahar Abdel-Haq na Mohamed Fadl na Walid Al-Attar Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Misri kwa mpira wa miguu.
Na timu ya kitaifa ya Misri ilikuwa kama ifuatavyo:
Kipa: Mohamed El Shennawy.
Ulinzi: Ahmed Hegazy Mahmoud Hamdi "Al-Wansh", Ahmed Abul-Fotouh na Muhammad Hani.
Viungo wa kujihami: Amr Al-Sulaia na Mohamed Al-Neni
Uwanja wa kati: Abdullah Al-Saeed, Mahmoud Hassan (Trezegeh) na Ahmed Sayed (Zizo).
Safu ya kukera: Mustafa Muhammad.
Timu ya kitaifa ya mpira wa miguu ya Misri ya kwanza itakutana na mwenzake Togo leo Jumamosi , siku ya 14 mwezi wa Novemba katika raundi ya tatu katika mechi za kufikia Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazokaribishwa na Cameroon 2022.
Timu ya kitaifa ya Misri huvaa sare ya msingi "nyekundu, nyeupe na nyeusi", wakati wageni wanavaa sare za manjano.
Mechi kati ya Misri na Togo itafanywa upya mnamo siku ya 17 mwezi wa Novemba katika raundi ya nne kwenye Uwanja wa Kege huko Lomé, mji mkuu wa Togo.
Timu ya kitaifa ya Comoro inaongozwa kwa Kundi cha saba ikiwa na alama 5, Kenya inashika nafasi ya pili na alama tatu, Misri inashika nafasi ya tatu na alama mbili na Togo iko chini ya kundi katika nafasi ya nne na alama moja tu.
Comments