Pamoja na ushiriki wa watoto elfu 1500 kutoka nchi 25 ...Vijana na Michezo yaendelea na maandalizi ya Tamasha la "Watoto wa Ulimwengu wakutana ... Misri ni Moyo wa Ulimwengu"
- 2020-11-16 11:40:24
Katika mfumo wa maadhimisho ya Siku ya Watoto Duniani, Wizara ya Vijana na Michezo inaendelea na maandalizi yake ya utekelezaji wa toleo la pili la Tamasha la Kimataifa linalowaleta pamoja watoto wa ulimwengu, linalofanyika chini ya kaulimbiu "Watoto wa Ulimwengu Wakutana ... Misri ndio Moyo wa Ulimwengu."mnamo kipindi cha kuanzia 20 hadi 25 Novemba ya mwaka huu kutoka miaka 12 hadi 17, inayotekelezwa na usimamizi mkuu wa waanzilishi katika huduma, zaidi ya watoto elfu 1500, wanaowakilisha timu 32 kutoka nchi 25, wanashiriki katika shughuli za Tamasha la Kimataifa, pamoja na ushiriki wa watoto wa Misri kutoka kwa mikoa anuwai na wenye ulemavu, pia watoto wa jamii za kigeni wanaoishi Misri, na tamasha hilo litafanyika mwaka huu kupitia njia za elektroniki za mawasiliano kutokana na kutokuwa na uwezo wa kukusanya watoto kutokana na virusi vya Corona.
Jiji la michezo huko Asmarat litashuhudia sherehe ya ufunguzi, inayofanyika Ijumaa, Novemba 20 saa sita mchana, na shughuli za tamasha hilo ni pamoja na seti tofauti ya shughuli za kawaida pamoja na maonesho ya timu zinazoshiriki kutoka nchi tofauti za ulimwengu na kikundi cha warsha za sanaa na kiutamaduni katika muziki, kuimba, na harakati. Shughuli za michezo na semina za uhamasishaji,Kupitia timu zinazoshiriki kutuma video zao kupitia barua pepe kwenye tamasha, na timu ya vijana wanajitolea hupokea, na kisha video na kazi hizo huonyeshwa kwenye ukurasa wa tamasha kupitia ratiba iliyotangazwa, baada ya hapo tume la suluhisho la kimataifa lenye wasuluhishi watano kutoka nchi tofauti linazichukua, likiongozwa na mwanachama kutoka Misri ilihukumu kazi tatu bora kuamua nafasi tatu za kwanza za kushinda, na washiriki wote kutoka nchi tofauti za ulimwengu watapata cheti kilichoidhinishwa cha ushiriki.
Mwishoni mwa wiki, kutakuwa na mkutano mkondoni unaofanyika na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, pamoja na nchi zote, zilizohudhuria na kiongozi wa timu na wawili kutoka kila timu watahudhuria.
Tamasha hilo la ulimwengu ni moja ya hafla muhimu na hafla za kimataifa zinazotekelezwa kwa kiwango hiki cha umri, pamoja na idadi ya washiriki na idadi ya nchi zinazotamani kushiriki katika Tamasha la Kimataifa la Misri.ambapo mwaka jana, shughuli za tamasha hilo zilishuhudia athari nzuri katika vyombo vya habari vya Kimataifa tofauti tofauti, haswa kuhusu ujumbe wa Amani kutoka kwa watoto Ulimwenguni ambao ulirushwa kutoka nchi ya Misri kuelekea sehemu zote za ulimwengu.
Comments