Farida Osman ashinda medali ya dhahabu kwenye mashindano wazi ya kuogelea ya Marekani


Mwogeleaji wa Misri Farida Osman alifanikiwa kutwaa medali ya dhahabu ya mashindano wazi ya kuogelea ya Marekani kwenye mbio za mita 50 kwa wakati wa 25.10 katika mafanikio ya kihistoria ya kuogelea kwa kimisri licha ya shida ya " Corona " iliyoenea Ulimwenguni na kuathiri michezo yote. Mwogeleaji Marwan Al-Qamah alifikia mashindano ya Olimpiki ya Tokyo mnamo 2021 baada ya kuvunja rekodi ya kufuzu kwa mbio za mita 800 muda wa mapumziko, akishinda nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya kuogelea  wazi ya Marekani.


Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliwapongeza Farida Osman baada ya kushinda dhahabu kwenye ubingwa wa Marekani, Marwan  Al-Qamah, mchezaji wa kufikia Olimpiki, pamoja na Shirikisho la kuogelea la Misri kwa juhudi zilizofanywa kwa njia ya mazoezi, maandalizi ya wachezaji kwa mashindano ya kitaifa na kufanikiwa kwao kwa matokeo ya kushangaza katika mashindano tofauti.


Waziri huyo alionesha kuunga mkono mashirikisho ya michezo kwa kushirikiana, kamati ya olimpiki ya Misri na kuunga mkono wachezaji wote wa kiume na wa kike na kufuata maandalizi yao ya mashindano tofauti kwa kuzingatia kwa kuendelea na mafanikio yaliyoshuhudiwa na mchezo wa Misri katika kipindi cha kisasa.


Mwogeleaji Farida Osman aliamua kurudi kwa ushiriki wa mashindano ya kimataifa licha ya shida ya Corona iliyoenea  ulimwenguni na alionesha furaha yake kwa kurudi. Na alisema kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii : Nina furaha na msisimko kwamba nitarudi tena kwa mashindano.

Farida alithibitisha kuwa atashiriki katika mashindano ya " Wazi ya Marekani" yatakayofanyika Greensboro, North Carolina atakaposhiriki, kama alivyosema, katika mbio za mita 50, mita 100 za fremu na mita 100 za kipepeo,  kesho, kisha kushiriki mbio za mita 50 za fremu na mita 100 za kipepeo na kumaliza ushiriki wake shindana katika mbio za mita 100.


Ikumbukwe kwamba Farida Osman alivunja rekodi kwenye mashindano ya " Tyrproswimseries " mwaka jana na akashinda medali ya dhahabu katika kipepeo cha mita 50 na muda wa 25,65.


Comments