" Hali ya kisasa ni bora zaidi katika uwanja wa Kairo"... Shirikisho la kimataifa la mpira wa mikono lasifu ukumbi na uwezo wake

 Ujumbe kutoka Shirikisho la mpira wa mikono la kimataifa ulitembelea ukumbi wa uwanja wa Kairo, siku 57 kabla ya kuanzia kwa toleo la 27 la mashindano ya mpira wa mikono Duniani kwa wanaume_ Misri 2021.


Ujumbe huo ulielezea kushangazwa kwake, uwezekano wa ukumbi utakaoandaa mechi ya ufunguzi mnamo Januari 13 kati ya Misri na Chile na pia mechi nyingi za raundi ya kwanza, raundi kuu na mechi mbili za mwisho.


Wakati wa ziara hiyo, ujumbe huo uliambatana na mkurugenzi wa mashindano Hussein Labib na naibu wake Khaled Fathy, kwa upande wa Shirikisho la kimataifa, mkuu wa kamati ya ukaguzi Alaa Al Sayed , Wawakilishi wa kampuni ya SportFive inayohusika na utangazaji wa Runinga ya mashindano hayo na wakuu kadhaa na wajumbe wa kamati ndogo za kamati ya maandalizi ya mashindano hayo.


Sven Hark, mkurugenzi wa uzalishaji katika SportFive, alisema:" Hali ya kisasa kwa ukumbi ni bora zaidi ".


"Tunafurahi sana na ukumbi sasa uko tayari kuandaa mashindano kwa ufanisi kamili", akaongeza.


Ukumbi wa uwanja wa Kairo ndio ukumbi mkubwa zaidi kati ya kumbi nne zinazoandaa mashindano hayo, nazo ni uwanja wa mji mkuu mpya wa kiutawala, uwanja wa Oktoba 6, na uwanja wa Borg Al Arab .


Ukumbi huo unaweza kuchukua watazamaji elfu 17 na hapo awali ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya ulimwengu yaliyofanyika nchini Misri mnamo 1999.


Ukumbi huo hivi karibuni ulifanywa na mradi wa kuongeza ufanisi wake, uliosifiwa na ujumbe kabla ya mashindano hayo, ambapo mechi yao ya mwisho itakapochezwa Januari 31 ijayo.

Comments