Vijana na Michezo yajadili maandalizi ya kiutendaji pamoja na Wizara za Utalii na Mambo ya Kale kwa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi
- 2020-11-26 15:14:36
Wizara ya Vijana na Michezo ilifanya mkutano pamoja na ujumbe wa Wizara za Utalii na Mambo ya Kale; Kujadili njia za ushirikiano wa pamoja kuhusu utekelezaji wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika, unaoamuliwa kutekelezwa mnamo robo ya kwanza ya 2021.
Mkutano huo ulionesha pande muhimu zaidi za ushirikiano kati ya Ofisi ya Vijana ya Afrika kwenye Wizara ya Vijana inayohusika na utekelezaji wa Udhamini huo pamoja na Wizara za Utalii na Mambo ya Kale, ambazo ni pamoja na kuweka vivutio vya kiutalii na ya akiolojia vinavyoweza kujumuishwa katika ajenda ya Udhamini ili kuwawezesha vijana waafrika wanaoshiriki kujua zaidi kuhusu vivutio vya kiutalii na kiutamaduni nchini Misri, pamoja na kujadili michango ya Wizara za Utalii na mambo ya kale kwa kuunga mkono udhamini huo kupitia kampuni za kitaifa za Misri, na uuzaji kupitia Mamlaka ya Kukuza Utalii, iliyokuwa na mchango mkubwa katika shughuli za kundi la kwanza.
Imekubaliwa pia kuingiza filamu za maandishi zilizoandaliwa na Mamlaka ya Utalii ya Misri ndani ya mpango wa Udhamini, na kuipa Makumbusho makubwa ya kimisri kipaumbele cha juu wakati wa mpango wa utalii, yalizingatiwa mradi mkubwa wa kitaifa.
Wawakilishi wa Wizara za Utalii na Mambo ya Kale walisema kuwa wataangalia mawazo mapya na ya kuchochea yanayokuza mchango wa utalii wa Misri na kuisambaza ndani na nje kupitia wapokeaji wa Udhamini kutoka nchi za Kiafrika na kuwafanya wawe mabalozi wa Misri huko kwao wakati wa kurudi kwao tena. Na kuangalia utaratibu wa kulishirikisha Shirika la Utalii la Afrika katika Tukio hilo muhimu linalosaidia Udhamini wa kiafrika.
Kwa upande wao, Timu ya Ofisi ya Vijana ya Afrika ilisifu mchango wa Wizara za Utalii na Mambo ya Kale wakati wa utekelezaji wa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser, pamoja na Programu ya kujitolea kwa Umoja wa Afrika, haswa kikao kilichotolewa na Waziri wa Mambo ya Kale Dokta Khaled Al-Anani, kwa mahudhurio ya Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Bibi Aya Shabi, Mjumbe wa Vijana waafrika mnamo Desemba 2019 kwenye Kituo cha Olimpiki huko Maadi.
Ikumbukwe kuwa Wizara ya Vijana na Michezo ilitekeleza kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika mnamo Juni 2019 chini ya uangalifu wa Waziri Mkuu Dokta Mostafa Madbouly, miongoni mwa shughuli za Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika 2019, zilizoagizwa na Rais El-Sisi wakati wa Mkutano wa Vijana Ulimwenguni. Na Udhamini wa Nasser ni Udhamini wa kwanza wa Kiafrika kuhamisha uzoefu wa maendeleo wa Misri kwa viongozi vijana watendaji barani, mbali na ni moja ya njia za kuamsha Hati ya Vijana wa Afrika, Ajenda ya Afrika 2030, na Ushirikiano wa Kusini-Kusini.
Comments