Wizara ya Vijana na Michezo, pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), zilisherehekea Siku ya Mtoto Duniani 2020, Na kupita kwa miaka thelathini na moja tangu Mkataba wa Haki za Mtoto, katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Jeremy Hopkins, Mwakilishi wa UNICEF huko Misri na Baraza la Kitaifa la Utoto na Akinamama, na ushiriki wa watu wengi wa kimichezo.
Dokta Ashraf Sobhy alisifu ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia utekelezaji wa mipango, ikiwa ni pamoja na mpango wa Michezo kwa ajili ya maendeleo na mpango wa safari wa mafunzo ya vijana na ukuzaji wa ujuzi, na kupa fursa kwa wasichana, haswa wasichana wa Misri ya juu, kufanya mazoezi ya michezo na kufanya mchezo kuwa njia ya maisha, akiashiria kuwa ilikubaliwa kushirikiana na Shirika hilo la UNICEF katika kuweka mkakati wa maendeleo ya michezo.
Jeremy Hopkins, Mwakilishi wa UNICEF huko Misri alisema: "wakati wa sherehe kwa Siku ya Mtoto Duniani, tunakutana pamoja ili kufanya upya ahadi yetu kufanya kazi kwa maendeleo wa haki za watoto na ulinzi wao, na ni muhimu sana kwa UNICEF kuunga mkono haki ya watoto na vijana kwa maisha na ukuaji , na kufanya kazi ya kuwawezesha na kuhimiza ushiriki wao.
Waziri wa Vijana na Michezo na mwakilishi wa UNICEF huko Misri walishiriki mazungumzo na watoto wanaoshiriki katika sherehe hizo na kuwasikiliza, wakipeleka ujumbe wazi kwamba upatikanaji wa michezo kwa aina zote ni haki kwa kila mtoto.
Sherehe hiyo pia ilishuhudia ushiriki wa watoto katika shughuli tofauti , michezo ya burudani na michezo, pamoja na kuwepo kwa kikundi cha watoto wenye ulemavu, na idadi kadhaa ya watoto kutoka familia wanaokuja Misri.
Comments