Sobhy ashinda tuzo ya Mtu Bora wa Mwaka kwa utamaduni wa Kiarabu


 Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na Mkuu wa Ofisi ya kiutendaji ya Mawaziri wa Kiarabu wa Vijana na Michezo, alishinda tuzo ya Mtu wa Utamaduni wa Michezo wa Mwaka katika kiwango cha Kiarabu.


 Baada ya mashindano makubwa kwa haiba nyingi za Kiarabu ambazo zina athari katika uwanja wa vijana na michezo, Kamati Kuu inayosimamia Shirikisho la Kiarabu la Utamaduni wa Michezo iliamua mashindano hayo kwa niaba ya Waziri Mmisri, kwani alichaguliwa kushinda tuzo hiyo kulingana na vigezo vilivyowekwa mnamo 2017 wakati wa kuanzishwa kwa Shirikisho la Utamaduni wa Michezo ya Kiarabu,  linalojumuisha  Mwanahabari Ashraf Mahmoud kutoka Misri (Mwenyekiti) _ Fawaz Al-Sharif kutoka Saudi Arabia (Makamu wa Kwanza) _ Abd al-Latif Al-Mutawakel kutoka Morocco (Naibu wa pili) _ Dokta Ahmed Saad Al-Sharif kutoka Emirates _ Muhammad Ismail kutoka Bahrain _ Salem Bin Sulayem Al-Kabeer kutoka Oman _  Lotfi Al-Abed kutoka Tunisia - Hassan Sharara kutoka Lebanon - Dokta Sabaa Jarrar kutoka Palestina - na Mwandishi wa habari Ayman Badra kama Katibu Mkuu.


 Ikumbukwe kwamba sherehe ya mwaka jana ilifanyika katika jiji la Dubai, UAE, na Sheikh Isa bin Rashid Al Khalifa kutoka Bahrain na watu wengi waarabu waliheshimiwa.

Comments