Waziri wa Michezo akutana na Kamati iandaayo Mashindano ya Mpira wa mikono Duniani

Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na kamati iandaayo Mashindano ya Mpira wa mikono Duniani, kwa mahudhurio ya  Mhandisi Hisham Nasr, Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Mikono la Misri na  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo na Hussein Labib Mkurugenzi wa Mashindano hayo, katika mfumo wa mikutano ya kila wiki ya mara kwa mara iliyofanywa na Waziri wa Vijana na Michezo ili kujua maandalizi ya mwisho ya kuandaa  mashindano na kuyatolewa  kwa muonekano mzuri kwa sifa na nafasi ya  Misri ulimwenguni.


Mkutano huo ulijadili majadiliano kwenye tiketi zitakazotolewa kwa mashabiki , kadi za kushangilia, pamoja na mchakato wa kuingia na kutoka kwa mashabiki na taratibu zao.



 Sobhy alisisitiza kuwa kipaumbele kinakuja katika mchakato wa kuhakikisha kuingia na kutoka kwa mashabiki , pamoja na kufuata hatua muhimu za tahadhari na kinga ili kusaidia mashabiki  watakaohamasisha timu ya kitaifa ya Misri wakati wa mashindano yake.



Akiongeza kuwa kamati hiyo inajadili maelezo yote ya mashindano ili kumaliza kwa wakati maalumu kutoka maelezo yote ya mashindano yaliyopangwa kufanyika Januari ijayo.


Mkutano huo ulihudhuriwa na Dokta Ahmed Al Sheikh, Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano ya Serikali ya Mashindano, Mohamed Diab Mshauri wa sheria kwa Waziri wa Vijana na Michezo, Magdy Rushdie Wakili wa Wizara hiyo na Mkuu wa Idara Kuu ya Huduma za usaidizi kwenye Wizara ya Vijana na Michezo, na wawakilishi wa kampuni ya Tiketi Yangu.

Comments