Waziri wa Michezo atafuta pamoja na maafisa wa kifedha na CAF Njia za kuanzisha makubaliano ya makao makuu ya CAF huko Kairo


 Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alitafutia na wawakilishi wa Wizara ya kifedha na kwa mahudhurio ya maafisa wa Shirikisho la Soka la Afrika, "CAF";  Njia za kuanzisha makubaliano ya makao makuu ya CAF na vifaa vyote vya kifedha na vifaa kwa makao makuu ya CAF huko Kairo.


Waziri wa Michezo alisisitiza kuwa Misri inataka kuwezesha kazi ya CAF kuendelea , kukuza na kuboresha umaarufu wa mpira wa miguu  barani  Afrika, akisisitiza kuunga mkono kwake makubaliano yaliyofikiwa kati ya Shirikisho la Afrika na serikali ya Misri, kwa kushirikiana na wizara za vijana na michezo, fedha, na wadau wengine  wa serikali.


Dokta Ashraf Sobhy aliwahakikishia ujumbe wa CAF ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Afrika Abdel Moneim Bah, kwamba makubaliano hayo yamekuwa yakitekelezwa na kulingana na masharti yake, mafanikio kadhaa yameongezwa kwa makao makuu ya CAF, maafisa wake na wafanyikazi, Ili kuwezesha  utendaji wa kazi za Shirikisho la Soka la Afrika huko Misri, makubaliano hayo pia yanajumuisha mafanikio ya kodi na ushuru wa forodha ambao utafurahiwa na makao makuu huko Misri.


Mkutano huo ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa CAF Abdel Moneim Bah, na ujumbe wa kiwango cha juu, na kutoka  Wizara ya Vijana na Michezo, Dokta Ahmed Al-Sheikh, Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara hiyo, na kikundi cha viongozi wa Wizara wanaojali walihudhuria.

Comments