Vijana na Michezo yahitimisha tamasha la "Watoto wa Dunia wanakutana ... Misri ni Moyo wa Dunia ", kwa ushiriki wa watoto 1500

 Dokta Ashraf Sobhy,Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia kumalizika kwa shughuli za tamasha la Siku za Watoto, lililotekelezwa na Wizara hiyo chini ya kauli mbiu "Watoto wa Dunia wanakutana .. Misri ni Moyo wa Dunia ", kwa ushiriki wa watoto 1500 kutoka nchi 30 kwa kikundi cha umri kutoka miaka 12 hadi 17, na hivyo ilikuwa kupitia mkutano wa video (Conference) katika kipindi cha kuanzia Novemba 26  Hadi Desemba 4.


Timu 45 zinazowakilisha nchi 30, pamoja na timu 10 kutoka Misri, zilishiriki katika tukio hilo na Watoto wa mji wa Asmarat wanashuhudia na wanashiriki katika shughuli kadhaa, "Tunaweza  kwa Tofauti - Watoto wasio na Nyumba , katika utekelezaji wa Mkakati wa Maendeleo Endelevu ya Misri 2030 kupitia mipango ya vikundi tofauti vya vijana, raia wa kesho.


 Kwa upande wake, Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kuwa tamasha hilo linawakilisha moja ya zana muhimu zaidi ya Wizara ya Vijana na Michezo kuwasiliana na watoto wa ulimwengu na kuunda mazingira ya uelewa na kubadilishana uzoefu na nchi tofauti za ulimwengu,akiashiria  umuhimu wa upanuzi katika kipindi kinachokuja cha kufanya mikutano na tukio nyingi  linalowakutanisha  vijana wa Misri na wenzao kutoka nchi tofauti za ulimwengu. ili kuthibitisha mahusiano ya ushirikiano na mahusiano ya pamoja na kuwapa uzoefu zaidi, kuwatambulisha na kuwafungulia tamaduni tofauti kutoka nchi zote za ulimwengu.


Shughuli za sherehe zilijumuisha vikundi tofauti ya shughuli kama vile maonyesho kwa timu zinazoshiriki kutoka nchi tofauti za ulimwengu na kikundi cha warsha za sanaa na utamaduni katika muziki, kuimba, utendaji wa harakati, shughuli za michezo na semina za uhamasishaji, kupitia timu zinazoshiriki kutuma video zao kupitia barua pepe ya tamasha, ambayo ilipokelewa na timu ya vijana wanaojitolea, Video na kazi hizi zilioneshwa kwenye ukurasa wa tamasha kulingana na ratiba iliyotangazwa, ambapo badaye kamati ya majaji ya kimataifa 

 walio na wasuluhishi 5  kutoka nchi tofauti wakiongozwa na mwanachama kutoka Misri walishughulikia ili kuchagua kazi 3 bora kuainisha nafasi ya kwanza ya kushinda, na washiriki wote kutoka nchi tofauti za ulimwengu watapata cheti cha ushiriki kilichoidhinishwa.


Tamasha hilo la kimataifa ni moja ya hafla muhimu sana ambayo hutekelezwa kwa umri huo, pamoja na idadi ya washiriki na nchi zinazotamani kushiriki kwenye tamasha hilo, kwani shughuli za tamasha hilo mwaka jana zilishuhudia athari nzuri katika Vyombo vya habari tofauti za kimataifa, haswa kwa habari ya ujumbe wa amani kutoka kwa watoto wa ulimwengu, uliotangazwa kutoka  Misri.

Comments